Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, Asasi za kiraia na wakazi wa karibu na maeneo ya fukwe ya Coco leo 6 Septemba, 2025 wamefanya usafi wa fukwe ya Coco ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Kampeni ya 'NEMC Usafi Kampeni' iliyozinduliwa rasmi 4 Septemba, 2025.
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, Mhandisi wa Mazingira (NEMC) Bw. Joshua Muro amesema NEMC ipo tayari kushirikiana na jamii pamoja na Asasi za kiraia katika kutekeleza Kampeni hiyo ya 'NEMC Usafi Kampeni' yenye lengo la kuhamasisha jamii kusafisha na kuhifadhi Mazingira, Pia ameitaka jamii kubadili mtazamo juu ya jukumu la usafi wa Mazingira na kufafanua kuwa ni jukumu la kila mmoja kufanya usafi wa Mazingira yanayomzunguka.
Baadhi ya watumishi wa NEMC na DEPO wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya zoezi la usafi katika Fukwe ya CocoKwa upande wake Mkurugenzi wa Asasi ya DEPO, Ndugu. Humphrey Milinga amesema lengo kubwa la zoezi hilo ni kuhamasisha jamii katika ngazi ya familia kusafisha Mazingira na kujumuika katika vikundi vya usafishaji Mazingira zikiwemo Fukwe.
Washiriki wengine walio jumuika katika zoezi hilo ni Africraft, MBC, WWF, TIA, TESCAR na Bethlehem Parish.
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira linaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa Mazingira na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Asasi za kiraia pamoja na wadau wengine ili kuhakikisha nchi yetu inakuwa na safi na salama kwa ustawi wa Afya na Mazingira.
Baadhi ya wakazi wa maeneo ya jirani na Fukwe ya Coco na baadhi ya watumishi wa NEMC kisafisha Fukwe hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni