Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limewataka wadau wa maonesho ya 49 ya kibiashara (sabasaba) kwa mwaka huu kudhibiti kelele chafuzi au sauti zinazozidi viwango na mitetemo kwenye mabanda wakati wa maonesho.
Kauli hiyo imetolewa Juni 26,2025 na Bw. Haji Kiselu, Mhandisi mwandamizi kutoka NEMC, kwenye semina ya awali ya maonesho, wakati wa wasilisho la athari za kelele chafuzi na mitetemo kwa wadau washiriki wa maonesho ya msimu wa sabasaba kwa mwaka 2025, yenye kauli mbiu isemayo " Maonesho ya 49 ya biashara ya Kimataifa, fahari ya Tanzania " yanayotarajiwa kuanza tarehe 28 Julai mwaka huu.
Amesema kelele chafuzi zinamadhara mengi yakiwemo kupoteza uwezo wa kusikia, kuharibu mahusiano ya jamii, kukosa kupumzika, kusababisha ajali na kwa kinamama kuweza kuharibika kwa mimba.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Albert Chalamila alipokuwa akihutubia aliwataka wadau hao kuzingatia biashara zinazosimamia na kuhifadhi mazingira kwani ndio msingi wa maendeleo endelevu ya uchumi wa kati hasa ikizingatiwa ndio agenda kubwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhifadhi na kusimamia mazingira nchini.
Awali akijibu swali lihusulo kelele nyakati za maonesho, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Mohamed Khamis amesema kwa kushirikiana na NEMC watahakikisha masuala ya kelele chafuzi na mitetemo yanadhibitiwa ili kuleta tija na maana halisi ya fahari ya watanzania katika maonesho hayo ya 49 ya kibiashara maarufu kwa jina la sabasaba
![]() |
| Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Mohamed Khamis akihutubia. |
![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Albert Chalamila alipokuwa akihutubia |
.jpeg)





.jpeg)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni