Timu ya wataalam wa Sayansi ya bahari kutoka Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambaye ni mratibu wa WIOMSA wameshiriki kongamano la wadau wa masuala ya bahari lililohusisha Watunga sera, wanasayansi ya bahari, wanasheria, wahandisi wa Mazingira, wanauchumi, wafanyabiashara, watafiti, wanavyuo na wazawa wanajamii ya pwani ambao ni wanachama wa Jumuiya ya Wanasayansi ya bahari magharibi mwa Bahari ya Hindi kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala ya Uhifadhi wa bahari ya Hindi.
Kongamano hilo la kumi na tatu (13 WIOMSA scientific symposium) limefanyika kuanzia tarehe 27 Septemba mpaka 3 Oktoba 2025 Mombasa nchini Kenya.
Ushiriki wa Baraza kwenye kongamano hilo kumesaidia kuongeza uelewa au kukuza taaluma ya Sayansi ya Bahari kwa wataalam wa bahari katika nyanja za Uhifadhi wa Mazingira, kupata fursa za kukutana na wadau wanaotoa fedha za kusaidia miradi au tafiti za Mazingira ya Bahari na Bioanuai zake pamoja na kupata taasisi na mashirika mbalimbali ya kushirikiana katika tafiti na miradi ya Uhifadhi wa Mazingira ya Bahari.
Aidha ushiriki huo pia utasaidia kuanzisha na kuimarisha mashirikiano kati ya Maafisa/Wanasayansi ya Bahari katika nchi za ukanda wa Magharibi ya Bahari ya Hindi, kutambua fursa za uwekezaji katika tafiti, teknolojia, biashara na uwekezaji katika sekta ya Uchumi wa Buluu pamoja na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi wanachama wa WIOMSA.
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi (wa pili kulia) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa WIOMSA Dkt.Arthur Tude na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo
Picha mbalimbali za washiriki wa Kongamano hilo zikijumuisha watumishi wa NEMC na wa WIOMSA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni