Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa mteja yenye kaulimbiu " Mission Possible" limeweka banda maalum katika ofisi zake ili kurahisisha huduma kwa wateja wake moja kwa moja.
Banda hilo limelenga kuboresha mawasiliano na kujenga mahusiano bora yenye kutoa fursa kwa wadau kutoa maoni, changamoto, pamoja na kupatiwa majibu ya papo kwa papo kuhusu huduma za mazingira.
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi akiwa katika banda maalum la kuhudumia wateja lililopo Ofisi za NEMC katika msimu wa Wiki ya Huduma kwa Mteja inayoadhimishwa kuanzia tarehe 6 hadi 10 Oktoba, 2025
Wateja waliofika Ofisi za NEMC wakipatiwa huduma katika Wiki ya Huduma kwa Mteja
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha (NEMC) Bw. Dickson Mjinja akifuatilia utoaji wa huduma kwa wateja waliofika katika banda maalum la NEMC katika Maadhimisho ya Wiki ya huduma kwa Mteja
Katika hatua nyingine Baraza Kupitia Kanda zake 13 limeendelea kutoa elimu ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira kwa wanachi
Ikiwa ni pamoja na kufanya ziara za ukaguzi (site visits) kwa wadau wake kujiridhisha na utekelezaji wa Kanuni za mazingira na kushughulikia changamoto zinazoibuliwa na wananchi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni