Nyumbani

NEMC YAFUTURISHA SERENA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali -Mgeni rasmi 

Aahidi Ushirikiano wa Kisheria katika Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeungana na wadau wa mazingira katika hafla ya futari iliyoandaliwa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kuendeleza mahusiano mazuri baina ya taasisi hiyo na wadau wake.

Hafla hiyo imefanyika Leo 26, 2026 katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi, watumishi wa Serikali na wadau binafsi walihudhuria tukio hilo lenye taswira ya umoja na mshikamano.

Akiongea katika hafla hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Hamza S. Johari  aliipongeza NEMC kwa kuandaa tukio hilo lenye kujenga umoja na kukuza mshikamano miongoni mwa Taasisi za Serikali na wadau wa mazingira. Aidha, aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa kisheria ili kuhakikisha Sheria na Kanuni za mazingira zinatekelezwa ipasavyo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi, alipozungumza alisema futari hiyo ni sehemu ya utamaduni wa Baraza katika kujenga uhusiano wa karibu na wadau wake.

Alisisitiza umuhimu wa kudumisha maadili ya utu, heshima na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya hifadhi ya mazingira nchini, akibainisha kuwa kupitia ushirikiano huo malengo ya kulinda na kuboresha mazingira yanaweza kufikiwa kwa ufanisi zaidi.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Abdul Rajabu Mhinte, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya NEMC na Ofisi ya Mkoa katika kusimamia na kutekeleza Sheria za mazingira. Aliahidi kuwa Ofisi ya Mkoa itaendelea kuunga mkono juhudi za uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira kwa ustawi wa taifa.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na wadau wa mazingira wakiwemo JMAT, Bodi ya NEMC, watumishi wa Baraza, wawakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Taasisi za kibenki









NEMC YASHIRIKI ZIARA YA NAIBU WAZIRI DKT. FESTO DUGANGE MABWEPANDE NA PUGU KINYAMWEZI

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limeshiriki ziara ya Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Festo Dugange ya kukagua Kiwanda cha kuzalisha mbolea ya mboji cha Mabwepande Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na Dampo la kukusanyia taka la Pugu Kinyamwezi Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo Mhe. Waziri Dkt. Festo Dugange amehimiza wananchi kuyatumia madampo kukusanyia taka ili zitumike kama malighafi pamoja na kusafisha mazingira.


Aidha, ameilelekeza NEMC kuendelea kusimamia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ili kuhakikisha Mazingira yanalindwa na kuhifadhiwa huku akitilia mkazo eneo la Usimamizi  wa taka za plastiki na kuzuia kelele chafuzi kutoka viwandani  na sehemu  za starehe. 

Amesema taka za plastiki katika madampo zimekuwa nyingi hali inayonesha pamoja na kupigwa marufuku uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa mifuko hiyo bado inaonekana


Aidha kutokana na kuwa asilimia 60 ya taka ni zinazozalishwa na kutupwa katika madampo ni zile zinazooza, aliwahimiza wananchi kutumia fursa hiyo kuzikusanya kwa ajili ya kutengeneza mbolea ya asili.

Pia Mhe Waziri amesisitiza  uanzishaji  wa viwanda  wa kuchakata taka  zisizooza kwa utengenezaji wa mbolea na Gesi.


Ziara hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saadi Mtambule na kwa upande wa NEMC imehudhuriwa na Kanda ya Mashariki Kusini upande wa ukaguzi wa Kiwanda cha kuchakata mbolea ya mboji cha Mabwepande na Kanda ya Ilala kwa upande ukaguzi wa Dampo la Pugu Kinyamwezi jijini Dar es Salaam.




NEMC YAFUTURISHA SERENA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali -Mgeni rasmi  Aahidi Ushirikiano wa Kisheria katika Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini Baraza la Taifa l...