Nyumbani

NEMC YASHIRIKI ZIARA YA NAIBU WAZIRI DKT. FESTO DUGANGE MABWEPANDE NA PUGU KINYAMWEZI

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limeshiriki ziara ya Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Festo Dugange ya kukagua Kiwanda cha kuzalisha mbolea ya mboji cha Mabwepande Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na Dampo la kukusanyia taka la Pugu Kinyamwezi Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo Mhe. Waziri Dkt. Festo Dugange amehimiza wananchi kuyatumia madampo kukusanyia taka ili zitumike kama malighafi pamoja na kusafisha mazingira.


Aidha, ameilelekeza NEMC kuendelea kusimamia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ili kuhakikisha Mazingira yanalindwa na kuhifadhiwa huku akitilia mkazo eneo la Usimamizi  wa taka za plastiki na kuzuia kelele chafuzi kutoka viwandani  na sehemu  za starehe. 

Amesema taka za plastiki katika madampo zimekuwa nyingi hali inayonesha pamoja na kupigwa marufuku uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa mifuko hiyo bado inaonekana


Aidha kutokana na kuwa asilimia 60 ya taka ni zinazozalishwa na kutupwa katika madampo ni zile zinazooza, aliwahimiza wananchi kutumia fursa hiyo kuzikusanya kwa ajili ya kutengeneza mbolea ya asili.

Pia Mhe Waziri amesisitiza  uanzishaji  wa viwanda  wa kuchakata taka  zisizooza kwa utengenezaji wa mbolea na Gesi.


Ziara hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saadi Mtambule na kwa upande wa NEMC imehudhuriwa na Kanda ya Mashariki Kusini upande wa ukaguzi wa Kiwanda cha kuchakata mbolea ya mboji cha Mabwepande na Kanda ya Ilala kwa upande ukaguzi wa Dampo la Pugu Kinyamwezi jijini Dar es Salaam.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NEMC YAFUTURISHA SERENA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali -Mgeni rasmi  Aahidi Ushirikiano wa Kisheria katika Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini Baraza la Taifa l...