Nyumbani

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR NI MGENI RASMI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA NEMC

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, mgeni rasmi Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 40 ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), yaliyofanyika Mei 29, 2026 katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mhe. Hemed ameipongeza NEMC kwa mchango wake mkubwa katika usimamizi na uhifadhi wa mazingira nchini kwa kipindi cha miaka 40 tangu kuanzishwa kwake. Amesema taasisi hiyo imeendelea kuwa chachu ya utoaji wa elimu ya mazingira, usimamizi wa sheria za mazingira pamoja na kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za uhifadhi wa mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa.

Aidha, amewataka Watanzania kuendelea kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira kwa kuepuka vitendo vinavyosababisha uharibifu wa mazingira na uchafuzi wa mazingira. Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali, taasisi mbalimbali na wananchi ni muhimu katika kuhakikisha mazingira yanaendelea kulindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.













Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

𝗡𝗘𝗠𝗖 𝗬𝗔𝗞𝗨𝗧𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗔 𝗪𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗔𝗝𝗜 𝗪𝗔 𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 𝗚𝗥𝗘𝗘𝗡 𝗦𝗨𝗠𝗠𝗜𝗧 𝟮𝟬𝟮𝟲

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na ujumbe wa waandaaji wa Tanzania Green Summit (TGS), inayotarajiwa ...