Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amezindua Kitabu cha Miaka 40 cha Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 40 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika mei 29, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe, Hemed ameipongeza NEMC kwa mchango wake mkubwa katika uhifadhi na usimamizi wa Mazingira nchini kwa kipindi cha miaka 40. Aidha ameeleza kuwa, Taasisi hiyo imeendelea kuwa nguzo muhimu katika kuhamasisha matumizi endelevu ya rasilimali za mazingira na kukabiliana na changamoto za uchafuzi wa mazingira pamoja na mabadiliko ya tabianchi.
Katika hayo, amewataka Watanzania kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za utunzaji wa mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, Taasisi binafsi na jamii katika kuhakikisha mazingira yanaendelea kuwa salama kwa maendeleo ya Taifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni