Nyumbani

NEMC YAMTUNUKU MHE. RAIS SAMIA TUZO YA MAZINGIRA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo maalum ya Mazingira kutokana na mchango wake mkubwa katika uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla,  kwa niaba ya Rais Dkt. Samia katika kilele cha maadhimisho ya miaka 40 ya NEMC yaliyofanyika JNICC, jijini Dar es Salaam.

Aidha, tuzo hiyo imetolewa ikiwa ni kutambua juhudi za Dkt. Samia katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na kampeni za kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji holela wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

Kupitia juhudi hizo, Dkt. Samia ameendelea kuhimiza wananchi kutumia nishati safi ya kupikia ili kulinda mazingira, kupunguza ukataji holela wa miti na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

𝗡𝗘𝗠𝗖 𝗬𝗔𝗞𝗨𝗧𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗔 𝗪𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗔𝗝𝗜 𝗪𝗔 𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 𝗚𝗥𝗘𝗘𝗡 𝗦𝗨𝗠𝗠𝗜𝗧 𝟮𝟬𝟮𝟲

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na ujumbe wa waandaaji wa Tanzania Green Summit (TGS), inayotarajiwa ...