Nyumbani

NEMC YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MAZINGIRA KATIKA MAONESHO YA SABASABA

Maafisa wa NEMC wakiendelea na kutoa mafunzo ya Mazigira kwenye maonesho ya SabaSaba 2025

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linaendelea kutoa elimu na huduma mbalimbali za mazingira katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Afisa wa NEMC akiendelea kutoa elimu ya mazingira kwa wageni waliotembelea banda la NEMC kwenye maonesho ya SabaSaba 2025

Ikiwa leo ni siku ya nne tangu kuanza kwa maonesho hayo, NEMC inaendelea kuwahamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira, madhara ya uchafuzi wa mazingira, pamoja na kusisitiza wananchi, wawekezaji na wafanyabiashara kutekeleza matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira.

Wageni kutoka nje ya nchi walifika kwenye banda la NEMC kupata elimu ya mazingira katika maonesho ya SabaSaba 2025

Katika banda la NEMC, wananchi wanapata fursa ya kuuliza maswali na kupata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Baraza, na namna bora ya kudhibiti taka na kelele kwenye maeneo ya makazi na biashara.

Baraza linaendelea kuwakaribisha wananchi wote kutembelea banda lake ili wapate maarifa sahihi yatakayowawezeshakuwa sehemu ya watetezi wa mazingira kwa maendeleo endelevu ya taifa letu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Sethi Ura Company Limited Yasimamia Mapinduzi ya Usafi: Ushirikiano wa Jamii Katika Kuweka Mazingira Safi Hospitali ya Wilaya ya Hai

Vijana wa kujitolea wakipanga majukumu kabla ya kuanza kazi ya usafi katika eneo la hospitali. Katika kuendeleza dhana ya afya bora inayoteg...