![]() |
Wajumbe wa NEMC wakiwakilisha Tanzania kenye mkutano wa Usimamizi wa Kemikali Uruguay 2025 |
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki Mkutano wa kwanza wa Kikosi Kazi kujadili Utekelezaji wa Mfumo Mpya wa Dunia wa Usimamizi wa Kemikali (Global Framework on Chemicals - GFC) uliofanyika jijini Punta del Este, nchini Uruguay kuanzia tarehe 22 hadi 27 Juni 2025. Aidha, Mkutano huo pia ulilenga kujadili na kuandaa mikakati ya utekelezaji, upatikanaji wa fedha, ushirikishwaji wa wadau, ufuatiliaji na tathmini ya utendaji wa nchi wanachama. Mkutano huo uliandaliwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), na Tanzania iliwakilishwa na taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Mamlaka ya Usalama Mahali pa Kazi (OSHA), pamoja na asasi ya kiraia ya Agenda for Action.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni