Nyumbani

SIMBACHAWENE AFUNGUA RASMI MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Waziri Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. George Simbachawene akizungumza katina maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mhe. George Boniface Simbachawene amezindua rasmi Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma ambayo yameambatana na maonesho yatakayofanyika kuanzia leo 17-23 Juni, 2025 katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho hayo Mhe. Waziri Simbachawene amesema kwa sasa kila mmoja ni shahidi wa mageuzi katika utendaji kazi ambapo mifumo mbalimbali ya kidigitali imeanzishwa na kurahisisha utendaji kazi na upatikanaji wa taarifa. 

Washiriki katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.

Watumishi wa Umma wakifuatilia kwa makini hotuba za uzinduzi, wakijizatiti kuleta mabadiliko chanya katika huduma za umma.
Picha ya pamoja ya viongozi walioshiriki uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.

    Waziri amebainisha baadhi ya mifumo ya kidigitali iliyoleta mageuzi katika utendaji ikiwa ni pamoja na mfumo e-Watumishi ambao umeleta ufanisi katika uandaaji wa mishahara na watumishi kupata haki zao kwa wakati,  Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi (e-Utendaji-PEPMIS) ambapo kila mtumishi wa umma anatakiwa kujaza utekelezaji wa shughuli anazofanya kila siku au kila wiki. 

    Pia mfumo wa Tathmini ya mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma (HR Assessment) unaowezesha kutambua mahitaji ya rasilimaliwatu katika utumishi wa umma na kuwafanya msawazo; na mfumo wa e-Mrejesho unaosaidia watumishi na wananchi kwa jumla kuwasilisha maoni, mapendekezo, kero na maulizo kwa Serikali haraka.

    Kwa upande wake Kaimu Meneja Kanda ya kati (NEMC) Bw. Novatus Mushi amesema katika maonesho hayo NEMC imejipanga kutoa elimu ya Mazingira na kuonesha huduma ambazo Baraza linazitoa kama ilivyo ada kuwa Siku hii hujikita kutoa elimu, kuonesha, kutoa huduma mbalimbali na kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni, mrejesho na changamoto mbalimbali zinazowakumba.

    Kaulimbiu iliyobeba Maadhimisho ya Wiki ya utumishi wa umma kwa mwaka 2025 ni "𝐇𝐢𝐦𝐢𝐳𝐚 𝐦𝐚𝐭𝐮𝐦𝐢𝐳𝐢 𝐲𝐚 𝐦𝐢𝐟𝐮𝐦𝐨 𝐲𝐚 𝐤𝐢𝐝𝐢𝐠𝐢𝐭𝐚𝐥𝐢 𝐢𝐥𝐢 𝐤𝐮𝐨𝐧𝐠𝐞𝐳𝐚 𝐮𝐩𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚𝐧𝐚𝐣𝐢 𝐰𝐚 𝐭𝐚𝐚𝐫𝐢𝐟𝐚 𝐧𝐚 𝐤𝐮𝐜𝐡𝐚𝐠𝐢𝐳𝐚 𝐮𝐰𝐚𝐣𝐢𝐛𝐢𝐤𝐚𝐣𝐢"

    Aidha, chimbuko la Sherehe hizi ni uamuzi wa Mkutano wa Mawaziri wenye dhamana ya Utumishi wa Umma uliofanyika mjini Tangiers Nchini Morocco mwaka 1994. Uamuzi huo ulizitaka Nchi za Afrika kusherehekea siku hii kwa kaulimbiu moja katika Bara zima la Afrika




 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Sethi Ura Company Limited Yasimamia Mapinduzi ya Usafi: Ushirikiano wa Jamii Katika Kuweka Mazingira Safi Hospitali ya Wilaya ya Hai

Vijana wa kujitolea wakipanga majukumu kabla ya kuanza kazi ya usafi katika eneo la hospitali. Katika kuendeleza dhana ya afya bora inayoteg...