Nyumbani

NEMC YAPIGA KAMBI SABASABA – YAWAKARIBISHA WANANCHI KUPATA ELIMU YA MAZINGIRA

 

Mhandisi Mwandamizi wa NEMC, Bw. Haji Kiselu akizungumza katika maonyesho ya sabababa.

    Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linashiriki Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba kwa kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wananchi wanaotembelea banda la lake lililopo katika Jengo la Karume.
    Akizungumza katika maonesho hayo, Mhandisi Mwandamizi wa NEMC, Bw. Haji Kiselu, amesema kuwa Baraza limejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa elimu ya mazingira inamfikia kila mwananchi, ili waweze kuelewa majukumu yao pamoja na Sheria inayolipa Baraza mamlaka ya kusimamia mazingira nchini.
    Kwa upande wake, Mhandisi wa NEMC, Bw. Peres Ntinginya, amesisitiza kuwa utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila mmoja, na ametoa wito kwa wananchi kutumia nishati safi ya kupikia kwa kuwa matumizi yake husaidia kulinda afya ya binadamu na viumbe hai, kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa, pamoja na kuhifadhi mazingira kwa ujumla.
    Naye mmoja wa wageni waliotembelea banda la NEMC, Mkazi wa Rufiji, Bw. Ayubu Njanja, amesema elimu aliyoipata kutoka kwa Maafisa wa Baraza imempa mwongozo sahihi wa kuzingatia utunzaji wa mazingira hasa katika shughuli za kilimo.
    NEMC inaendelea kutoa wito kwa wananchi kutembelea banda lake lililopo katika Jengo la Karume, Sabasaba, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, ili kupata elimu ya mazingira. Maonesho haya yanafanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2025, yakiwa na kaulimbiu isemayo: “Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa – Fahari ya Tanzania.”
 

Mwananchi akifurahia mafunzo ya mazingira kutoka NEMC Sabasaba! Hii ni hatua kubwa kuelekea maisha bora na mazingira yenye afya. #MazingiraBora #NEMC


NEMC Sabasaba inawakaribisha wananchi kupata elimu ya mazingira kwa njia ya furaha na ushirikiano. Mazingira bora, maisha bora! #NEMC #ElimuKwaWananchi


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Sethi Ura Company Limited Yasimamia Mapinduzi ya Usafi: Ushirikiano wa Jamii Katika Kuweka Mazingira Safi Hospitali ya Wilaya ya Hai

Vijana wa kujitolea wakipanga majukumu kabla ya kuanza kazi ya usafi katika eneo la hospitali. Katika kuendeleza dhana ya afya bora inayoteg...