Baraza za la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limefanikisha mafunzo ya kujenga uwezo wa kitaifa juu ya nyenzo za Usimamizi wa Mazingira nchini kwa Wizara, Taasisi na Mamlaka za Serikali za mitaa.
Mafunzo hayo ya siku mbili yalianza jana 20 Agosti, hadi leo 21, 2025 katika Hoteli ya Midland Jijini Dodoma huku yakihusisha uwasilishaji wa mada na majadiliano, pamoja na maswali na majibu ya papo kwa papo.
Aidha mafunzo hayo yalilenga kuhakikisha Taasisi zote za umma na Mamlaka za Serikali za mitaa zinahakikisha matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake yanatekelezwa ipasavyo
Afisa Mazingira Mkuu wa NEMC na Mratibu Mkuu wa Mradi wa EMA upande wa NEMC, Bw. Paul Mashaija Kalokola akizungumza katika Mafunzo hiyo
Baadhi ya mada zilizowasilishwa ni pamoja na hali ya udhibiti wa taka za kielekroniki katika miji na manispaa, changamoto na fursa zilizopo katika taka za kielektroniki, Udhibiti wa madampo haramu, Mpango mkakati wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira, Mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii pamoja na Kaguzi za Mazingira pamoja na mchakato wa kupata vibali vya taka hatarishi pamoja na changamoto zilizopo katika udhibiti wake.
Baadhi ya maafisa wa NEMC wakiwasilisha mada katika Mafunzo hiyo
Katika kuhitimisha mafunzo hayo baadhi ya washiriki wamelishukuru Baraza kwa mafunzo hayo huku wakieleza kuwa wamepata mbinu mpya ambazo awali hawakuwa nazo katika swala zima la Usimamizi wa Mazingira nchini.
Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni