Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) imepitishwa kwenye wasilisho maalum kuhusu Mfumo wa Kidijitali wa Kufuatilia Uchafuzi wa Mazingira ujulikanao kama Online Continuous Emissions Monitoring System (OCEMS).
Mfumo huu wa kisasa umeundwa kwa lengo la kufanikisha ufuatiliaji wa wakati halisi wa viwango vya uchafuzi vinavyotolewa na viwanda na sekta mbalimbali, hatua inayolenga kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika kusimamia mazingira nchini.
Kupitia mfumo huu, taarifa za uchafuzi wa hewa zitapatikana moja kwa moja na kwa wakati jambo ambalo litasaidia katika kufanya uamuzi sahihi kuhusu hatua za kudhibiti uchafuzi. Aidha, mfumo huu utawezesha kuimarika kwa ushirikiano kati ya wadau wa mazingira kwa kuwa taarifa zitakuwa wazi na zinazopatikana kwa urahisi, hivyo kuchochea jitihada za pamoja katika kulinda mazingira na afya ya jamii.
Bodi ya NEMC ikipatiwa Mafunzo ya mfumo wa ufuatiliaji wa Mazingira Kidigitali
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni