Nyumbani

NEMC YAWANOA MAWAKILI WA SERIKALI SHERIA YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa mafunzo ya uelewa wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na utekelezaji wa majukumu yake kwa mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria.

Akizungumza katika Mafunzo hayo tarehe 3 Septemba, 2025 Mkurungenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Semesi amesema kuwa wameandaa mafunzo hayo kwa lengo la kujengeana uelewa wa kisheria katika usimamizi wa mazingira nchini pamoja na kuboresha mahusiano mazuri katika Usimamizi na Utekelezaji wa Sheria za Mazingira nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi akizungumza katika Mafunzo hayo 

Akifungua Mafunzo hayo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amesema wanasheria hao wanatakiwa kuwa walinzi na kuongeza umakini katika kutoa ushauri wa sheria za mazingira kwa maslahi ya nchi.

"Natambua zipo changamoto wakati wa utekelezaji, mfano uelewa mdogo wa masuala ya mazingira hivyo tunawajibu wa kuzibadili changamoto hizi na kuzifanya fursa kwa kuimarisha nafasi ya NEMC katika kusimamia sheria katika sekta ya mazingira."Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amelishukuru Baraza na kueleza kuwa mafunzo hayo yataongeza uelewa kwa Mawakili wa Serikali hivyo kuwasaidia wakati watakapokuwa wanatoa Ushauri wa Kisheria na Upekuzi wa Mikataba inayohusu hifadhi na usimamizi wa mazingira nchini.

Baadhi ya Mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria wakifuatilia mafunzo hayo

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari akieleza jambo wakati wa Mafunzo hayo
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi akimweleza jambo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari mara baada ya Mafunzo hayo, Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha (NEMC) Bw. Dickson Mjinja na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Sheria NEMC, Bw. Joannes Karungura 

Picha ya pamoja mara baada ya mafunzo hayo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NEMC YASHIRIKI MKUTANO WA SABA WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU MAZINGIRA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linashiriki Mkutano wa Saba (07) wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (07th Unit...