Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na African Adaptation Initiative (AAI), limeandaa warsha ya siku tatu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wataalamu wake kuhusu mbinu bora za kupata na kusimamia fedha za miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo inafanyika kuanzia 26-28 Agosti, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa NEMC.
AAl, ambayo ilianzishwa na Wakuu wa Nchi za Afrika, inalenga kusaidia mataifa ya Bara la Afrika katika kuongeza uwezo wao wa kupata rasilimali za kifedha za kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
Kupitia mpango wake mahsusi uitwao Adaptation Project Incubator for Africa (APIA), AAl inasaidia taasisi na nchi wanachama kuboresha uandishi, uandaaji na utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Aidha, NEMC iliingia makubaliano ya ushirikiano (MoU) na AAl ili kuwezesha Tanzania kunufaika na fursa hii ya mafunzo. Warsha hii ni matokeo ya makubaliano hayo na inalenga kuimarisha uelewa wa wataalamu wa NEMC katika maeneo mbalimbali ikiwemo: Mifumo ya kitaasisi na kifedha kuhusu mabadiliko ya tabianchi, Uandishi na uwasilishaji wa Miradi ya kimataifa, Usimamizi wa utekelezaji wa miradi, na mbinu za kushiriki kikamilifu katika majadiliano ya kimataifa kuhusu fedha za miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Picha ya pamoja mara baada ya kuhitimishwa kwa Warsha ya siku tatu yakuwajengea uwezo wataalamu wa NEMC kuhusu mbinu bora za kupata na kusimamia fedha za miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi iliyofanyika kuanzia 26-28 Agosti, 2025
Kupitia mpango wake mahsusi uitwao Adaptation Project Incubator for Africa (APIA), AAl inasaidia taasisi na nchi wanachama kuboresha uandishi, uandaaji na utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Aidha, NEMC iliingia makubaliano ya ushirikiano (MoU) na AAl ili kuwezesha Tanzania kunufaika na fursa hii ya mafunzo. Warsha hii ni matokeo ya makubaliano hayo na inalenga kuimarisha uelewa wa wataalamu wa NEMC katika maeneo mbalimbali ikiwemo: Mifumo ya kitaasisi na kifedha kuhusu mabadiliko ya tabianchi, Uandishi na uwasilishaji wa Miradi ya kimataifa, Usimamizi wa utekelezaji wa miradi, na mbinu za kushiriki kikamilifu katika majadiliano ya kimataifa kuhusu fedha za miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Kupitia mafunzo haya, NEMC inatarajiwa kuongeza uwezo wake wa kuandaa na kusimamia miradi mikubwa ya kimkakati, hivyo kuisaidia Tanzania kuongeza fursa za kupata fedha za kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni