Mafunzo hayo ya siku nne yalifanyika kuanzia tarehe 18 hadi 21 Novemba 2025 yakilenga kuongeza weledi na kuimarisha utendaji katika kupitia taarifa na kufanya kaguzi za miradi inayowasilishwa kwa Baraza, kuimarisha umahiri wa watumishi hao na kuandaa timu madhubuti yenye uwezo wa kushughulikia kwa haraka na kwa ubora wa juu taarifa za tathmini na kaguzi za mazingira zinazowasilishwa na wawekezaji kwa Baraza.
Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii (NEMC) Bi. Lilian Lukambuzi akiwasilisha mada katika mafunzo hayo
Mafunzo haya yalifunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii, Bi. Lilian Lukambuzi, na kuendeshwa na wataalamu kutoka ndani ya Kurugenzi hiyo wakiwemo Eng. Luhuvilo Mwamila "Kaimu Meneja Mapitio ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii" na Bi. Edika Masisi "Meneja Usajili wa Wataalamu Elekezi wa Mazingira". Washiriki walipata nafasi ya kujifunza kwa undani namna bora za kufanya mapitio ya taarifa za TAM, vigezo vya tathmini, na hatua muhimu katika ukaguzi wa mazingira ili kuhakikisha miradi inazingatia sheria ya Mazingira.Aidha, mafunzo hayo yaliwalenga watumishi wa NEMC kutoka kanda za Mashariki Kaskazini, Mashariki Kusini, Ilala, Temeke, Bagamoyo pamoja na Makao Makuu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni