Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI anayeshughulikia Afya Mhe. Dkt. Rajab Seif azuru Banda la NEMC katika maonesho ya kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo leo ni siku ya tatu tangu kufunguliwa kwake tarehe 1Juni, 2026.
WATUMISHI WA NEMC WAKITOA ELIMU YA MAZINGIRA KATIKA WIKI YA MAONESHO KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI, JUNI 2026
DKT. MKAMA AZURU BANDA LA NEMC MAONESHO YA KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI JUNI 5
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Switbert Zacharia Mkama (Mb)
ametembelea Banda la NEMC katika maonesho ya Maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma.
Aidha, Mhe. Naibu Waziri alipozungumza, ameitaka NEMC kuongeza nguvu katika udhibiti wa maswala ya uharibifu wa Mazingira ikiwa ni pamoja na uchomaji holela wa misitu. Pia kutoa elimu kwa makundi yote ya jamii kuanzia vijana mpaka wazee, ufuatiliaji wa misitu kupitia Kanda za NEMC, kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na kuhimiza usafi kwa mito inayokabiliwa na uchafuzi.
Elimu ya Mazingira ikitolewa katika banda la NEMC katika Kongamano la Vijana lililofanyika katika Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Juni 2, 2026 lenye kauli mbiu "Ushiriki wa Vijana katika Kutekeleza Dira 2050: Usimamizi Endelevu wa Mazingira na Uhimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi"
WAZIRI MASAUNI AZURU BANDA LA NEMC KONGAMANO LA VIJANA LILILOFANYIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Elimu ya Mazingira ikitolewa katika banda la NEMC katika Kongamano la Vijana lililofanyika katika Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Juni 2, 2026 lenye kauli mbiu "Ushiriki wa Vijana katika Kutekeleza Dira 2050: Usimamizi Endelevu wa Mazingira na Uhimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi"
NEMC YASHIRIKI KONGAMANO LA VIJANA KUJADILI USIMAMIZI ENDELEVU WA MAZINGIRA NA DIRA 2050
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeungana na wadau mbalimbali wa Mazingira kushiriki Kongamano la Vijana lililofanyika Juni 2, 2026 katika Ukumbi wa Maktaba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), likiwa na kaulimbiu isemayo "Ushiriki wa Vijana katika Kutekeleza Dira 2050: Usimamizi Endelevu wa Mazingira na Uhimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi."
Akifungua kongamano hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni, amesisitiza umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ili kuhakikisha maendeleo endelevu na utekelezaji wenye mafanikio wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Kupitia kongamano hilo, NEMC imepata fursa ya kutoa elimu ya mazingira kwa vijana, kuhamasisha matumizi endelevu ya rasilimali na kujadili nafasi ya vijana katika kuibua suluhisho bunifu za kukabiliana na changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa maendeleo ya Taifa ya sasa na vizazi vijavyo.
𝗡𝗘𝗠𝗖 𝗬𝗔𝗞𝗜𝗙𝗨𝗡𝗚𝗜𝗔 𝗞𝗜𝗪𝗔𝗡𝗗𝗔 𝗖𝗛𝗔 𝗦𝗔𝗡 𝗦𝗛𝗔𝗡 𝗡𝗔 𝗕𝗔𝗜-𝗟𝗬 𝗣𝗔𝗣𝗘𝗥 𝗖𝗢. 𝗟𝗧𝗗 𝗠𝗞𝗨𝗥𝗔𝗡𝗚𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗨𝗞𝗜𝗨𝗞𝗪𝗔𝗝𝗜 𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗘𝗥𝗜𝗔 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗭𝗜𝗡𝗚𝗜𝗥𝗔
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekifungia kiwanda cha SAN SHAN na BAI-LY PAPER CO. LTD kwa kukiuka sheria na ...
-
Ni katika kufanya tathmini na kuimarisha umoja. Watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Makao Makuu na k...
-
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linashiriki Mkutano wa Saba (07) wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (07th Unit...
-
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kusini tarehe 15 Novemba 2025 lilishiriki kusimamia na kushuhudia Uteke...