Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki mafunzo ya muda mfupi yaliyolenga kukuza uelewa kwa wataalamu katika umuhimu wa kutumia mbinu za Kijiografia (Geospatial Methods) kwenye uchambuzi wa taarifa za Kimazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi (Advanced GIS Training) yaliyoratibiwa na Shirika la Grumeti Fund Trust kupitia Programu ya Utafiti na Ubunifu kwa Mfumo Ikolojia wa Serengeti (Research and Innovation for the Serengeti Ecosystem-RISE).
Mafunzo haya yaliyoendeshwa kwa ushirikiano wa RISE, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Chuo Kikuu cha Pennsylvania na Chuo Kikuu cha Montana yamefanyika ndani ya Hifadhi ya Grumeti, Magharibi mwa Serengeti kuanzia tarehe 14 hadi 20 Julai, 2025.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni