Naibu katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Peter Msofe ametembelea Banda la NEMC lililoko viwanja vya Nanenane Nzuguni , Jijini Dodoma.
Akiwa bandani hapo, alifurahishwa na elimu ya Mazingira inayotolewa hususani ya namna bora ya kufanya kilimo, uvuvi na ufugaji unaozingatia utunzaji wa mazingira kwa mstakabali wa maendeleo endelevu nchini.
Amefurahishwa na huduma hiyo na kuitaka NEMC kuendeleza juhudi za utoaji elimu ya usimamizi na uhifadhi wa mazingira kwa mujibu wa Sheria
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira) Profesa Peter Msofe akizungumza na watumishi wa NEMC alipotembelea banda la NEMC leo 2 Agosti, 2025 katika maonesho ya wakulima (Nanenane 2025) yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni