Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki kikamilifu kwenye hafla ya ufungaji wa maonesho ya 32 ya wakulima (Nanenane) Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma leo
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo katika hotuba yake amesisitiza umuhimu wa kilimo bora na endelevu kama mhimili wa maendeleo ya Taifa.
Amesema sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi, hivyo zinahitaji uwekezaji wa kutosha, ubunifu na usimamizi madhubuti ili kuijenga kesho bora kwa Watanzania wote.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akiwasili katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma kufunga Maonesho ya Wakulima (Nanenane 2025) katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.
Ameelekeza Wizara ya Kilimo kuimarisha upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima, pamoja na kuunganisha nguvu katika kukuza sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.
Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametangaza kuongeza siku mbili zaidi za maonesho hadi tarehe 10 Agosti ili kutoa nafasi kwa wananchi na wadau kuendelea kupata huduma na elimu mbalimbali.
" Maonesho haya ni siku nane, lakini kiuhalisia siku nane hazitimii kwani maandalizi yanachelewa, hivyo kuanzia mwaka ujao maandalizi ya maonesho yaanze tarehe 25/07." Ameelekeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
Hafla hiyo ya ufungaji imehudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu, Wakuu wa Mikoa ya Dodoma na Singida, Wakuu wa Taasisi za Serikali na Binafsi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa hafla ya ufungaji wa Maonesho ya Wakulima (Nanenane 2025) katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.
Kwa upande wake, NEMC ilitumia maonesho haya kutoa elimu juu ya uhifadhi wa mazingira katika shughuli za kilimo na ufugaji, ikiwa ni pamoja na matumizi salama ya mbolea, upandaji miti, na ulinzi wa vyanzo vya maji.
Maonesho ya Nanenane mwaka huu yameendelea kuwa jukwaa muhimu kwa serikali, Taasisi na wananchi kushirikiana katika kuendeleza kilimo chenye tija na rafiki kwa mazingira.
Baadhi ya watumishi wa NEMC na Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwakatika hafla ya ufungaji wa maonesho ya wakulima (Nanenane 2025) katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni