Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetekeleza agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan la kuongeza muda wa kutoa huduma zake katika viwanja vya maonesho ya Nane Nane vilivyopo Nzuguni, Jijini Dodoma.
Hatua hiyo inalenga kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi, hususan wakulima na wafugaji wanaoshiriki maonesho hayo, ili kuwajengea uelewa na kuwasaidia kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira.
NEMC inaendelea kutoa elimu inayohusu masuala ya matumizi endelevu ya ardhi, uhifadhi wa vyanzo vya maji, na namna ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta ya kilimo na ufugaji.
Vilevile, wananchi wameelimishwa kuhusu taratibu za kupata vibali vya mazingira na umuhimu wa kufanya Tathmini ya athari kwa mazingira kabla ya kuanzisha miradi.
Baraza hilo linaendelea kuwakaribisha wananchi wote kutembelea banda lake ili kushirikiana kwa pamoja katika kusimamia na kuhifadhi mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa.
“Mazingira ni msingi wa maisha yetu. Tukiyaacha, na sisi tutapotea. Tushirikiane kuyatunza kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo,”
Elimu ya Mazingira ikitolewa kwa wageni waliotembelea banda la
NEMC katika maonesho ya wakulima, Nanenane 2025 katika Viwanja vya Nzuguni
jijini Dodoma katika siku za nyongeza ikiwa ni agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuongeza muda wa maonesho hayo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni