Nyumbani

NEMC, EWURA NA PAU ZAJADILI UWEKAJI WA MIFUMO YA UDHIBITI HEWA CHAFUZI KATIKA MRADI WA EACOP

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Tanzania (EWURA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Petroli Uganda (PAU) limefanya majadiliano ya kitaalamu na wataalam kutoka Mradi wa Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanga (EACOP) yaliyojikita katika usimikaji wa mifumo ya kudhibiti uchafuzi wa hewa inayosaidia kukusanya mvuke (Vapour Recovery Units – VRU) na hewa chafuzi zinazotokana na shughuli za usafirishaji, upakuaji na upakiaji wa mafuta.

Mifumo hiyo inalenga kulinda mazingira na afya za jamii zinazozunguka vituo mbalimbali vinavyotarajiwa kuwa na uzalishaji mkubwa wa gesi ya methane na gesi nyinginezo ndani ya mradi huo. 

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Baraza katika kuhakikisha kuwa miradi ya kimkakati inazingatia viwango vya ubora wa mazingira, hivyo kuchangia katika kulinda mazingira kwa maendeleo endelevu.







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

𝗡𝗘𝗠𝗖 𝗬𝗔𝗞𝗨𝗧𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗔 𝗪𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗔𝗝𝗜 𝗪𝗔 𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 𝗚𝗥𝗘𝗘𝗡 𝗦𝗨𝗠𝗠𝗜𝗧 𝟮𝟬𝟮𝟲

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na ujumbe wa waandaaji wa Tanzania Green Summit (TGS), inayotarajiwa ...