Nyumbani

NEMC YAUNGURUMA JNICC KONGAMANO LA ANWANI ZA MAKAZI

Yatoa Elimu ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira 

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa elimu ya mazingira kwenye Kongamano la Mwaka la Anwani za Makazi na Maonesho ya Teknolojia ya Huduma za Posta 2026 ihusuyo masuala mazima ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 na Kanuni zake katika  Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kongamano hilo linalotarajiwa kuhitimishwa Februari 08, 2026, Mhandisi Mkuu wa NEMC Bw. Jampyon Mbugi amesema kuwa matumizi sahihi ya anwani za makazi ni nyenzo muhimu katika kuimarisha usimamizi wa mazingira kupitia mfumo wa NAPA ambao utaiwezesha NEMC kupata taarifa muhimu za uhifadhi na usimamizi wa mazingira.

Ameongeza kuwa elimu hiyo inalenga kuwajengea wananchi uelewa wa majukumu yao ya kisheria na kijamii katika kulinda mazingira. Hata hivyo, anwani za makazi si utambulisho pekee wa maeneo bali ni chombo muhimu cha kupanga makazi na kusimamia mazingira kwa maendeleo yanayozingatia ustawi wa jamii na mazingira kwa ujumla. 

Naye Mhandisi Migodi NEMC, Bw. Hezron Mwashibanda ameeleza kuwa huduma zinazotolewa katika banda la NEMC ni pamoja na udhibiti wa kelele chafuzi, ufuatiliaji wa utekelezaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM/EIA), pamoja na utekelezaji wa Sheria, ada za mazingira katika maeneo ya makazi na biashara.

NEMC inawakaribisha wananchi na wadau wote wa mazingira kupata elimu ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NEMC YASHIRIKI KIKAMILIFU KONGAMANO LA ANWANI ZA MAKAZI NA MAONESHO YA TEKNOLOJIA ZA POSTA 2026

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki kikamilifu Kongamano la Mwaka la Anwani za Makazi na Maonesho ya Hud...