Nyumbani

BARAZA LA WAFANYAKAZI NEMC LAKUTANA

Lajadili Rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027

Baraza la wafanyakazi la NEMC limefanya Kikao maalum cha kujadili rasimu ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 kwa mujibu wa taratibu za uandaaji wa bajeti, likilenga kuimarisha uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji katika utekelezaji wake. 

Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi kimefanyika Februari 20, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa NEMC, Jijini Dar es Salaam, kikihusisha wajumbe ili kuchangia mawazo na mapendekezo yao.

Katika majadiliano, wajumbe walijikita katika masuala ya ustawi na maslahi huku mkazo mkubwa ukiwekwa kwenye kuongeza juhudi na maarifa kazini ili kuongeza mapato ya Baraza na pia kuendelea kutoa elimu ya Uhifadhi wa Mazingira kwa jamii, kwa lengo la kuimarisha utunzaji wa mazingira na kuchochea maendeleo endelevu ya Taifa.



















Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

𝗡𝗘𝗠𝗖 𝗬𝗔𝗞𝗨𝗧𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗔 𝗪𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗔𝗝𝗜 𝗪𝗔 𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 𝗚𝗥𝗘𝗘𝗡 𝗦𝗨𝗠𝗠𝗜𝗧 𝟮𝟬𝟮𝟲

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na ujumbe wa waandaaji wa Tanzania Green Summit (TGS), inayotarajiwa ...