Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC leo 30 Julai, 2025 limepiga maarufu zoezi la Uchimbaji mchanga katika bonde la mto Mpigi unaotenganisha Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani ambalo limekuwa likiharibu Mazingira na kuhatarisha makazi ya watu wa eneo hilo kutokana na mmomonyoko wa udongo.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa mto huo, Meneja Uzingatiaji wa Sheria NEMC Bw. Hamadi Taimuru amesema ni marufuku wote wanaojihusisha na Uchimbaji wa mchanga katika mto huo kwa kigezo cha kusafisha mto. Amewataka kuacha mara moja uchimbaji na kuwataka wafike katika Ofisi za NEMC ili wapatiwe vibali vyenye vigezo vya kusafisha mto na si Uchimbaji wa mchanga kwa mustakabali wa utunzaji wa Mazingira.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Baraza la wazee Bw. Lazaro Silla amesema kwa niaba ya wakazi wa eneo hilo hawahitaji Uchimbaji wa mchanga katika eneo hilo kwani unasababisha uharibifu wa Mazingira na kuhatarisha usalama wa makazi yao hivyo ameiomba NEMC kudhibiti swala hilo ili lisiendelee kuleta madhara.
Timu ya NEMC ikiwa katika ziara ya ukaguzi wa mto MpijiAidha, Bw. Taimuru ameongeza kuwa marufuku hii si tu kwa mto mpiji bali ni mito yote na maeneo yote nchini ambayo wanajihusisha na uchimbaji mchanga na kusababisha uharibifu wa Mazingira na kuhatarisha makazi ya watu.
Sambamba na hayo amesisitiza wote wanaojihusisha na Uchimbaji mchanga holela kote nchini kutii agizo hilo ili kuepusha uharibifu wa Mazingira na hatari ya kuharibika kwa makazi ili kujiepusha na adhabu kali inayoweza kutolewa.
Meneja Uzingatiaji wa Sheria (NEMC) Bw. Hamadi Taimuru akitoa maelekezo ya marufuku kwa baadhi ya wachimbaji mchanga katika mto Mpiji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni