Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lilipiga kambi viwanja vya sabasaba maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ili kutoa elimu ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa wananchi waliotembelea banda hilo katika Jengo la Karume.
Akizungumza katika maonesho hayo, Mhandisi Mwandamizi wa
NEMC, Bw. Haji Kiselu, alisema Baraza limejipanga kikamilifu kuhakikisha elimu
ya mazingira iliyo jumuishi inamfikia kila mwananchi, ili kwa pamoja tuweze
kuyasimamia kwa maendeleo endelevu nchini.
Kwa upande wake, Mhandisi wa NEMC, Bw. Peres Ntinginya,
alipozungumza, alisisitiza kuwa utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila mmoja
hivyo yapasa kuwajibika na kutoa wito
kwa wananchi kutumia nishati safi ya kupikia kwa kuwa matumizi yake husaidia
kulinda afya ya binadamu na viumbe hai, kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa,
pamoja na kuhifadhi mazingira kwa ujumla.
Bw. Ayubu Njanja akipatiwa elimu ya
mazingira kutoka kwa wataalam wakati wa msimu wa maonesho ya 49 ya Sabasaba.
Elimu ya Mazingira ikitolewa kwa wageni waliotembelea banda la NEMC katika maonesho ya 49 ya Sabasaba 2025
Elimu ya Mazingira ikitolewa kwa wageni waliotembelea banda la NEMC katika maonesho ya 49 ya Sabasaba 2025
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni