Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limeshiriki Mkutano wa kamati ya kimataifa ya majadiliano ya kuanzisha mkataba wa kimataifa wa kukabiliana na uchafuzi unaotokana na Plastiki nchini nchini Uswisi mjini Geneva
Mkutano huo umehusisha jopo la wadau wa Mazingira kutoka nchini Tanzania likiongozwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) profesa Peter Msofe, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, maafisa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, NEMC, TBS, na GCLA ambao walishiriki kikamilifu kwa siku zote kumi za majadiliano ya kuanzishwa Mkataba huo.
Meneja wa Uzingatiaji wa Sheria (NEMC) Bw. Hamadi Taimuru akiwasilisha mada katika Mkutano huoNaibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Peter Msoffe (wa kwanza kulia) na Bw. Hamadi Taimuru (wa pili kushoto) wakifuatilia Mkutano huo
Hata hivyo kutokana na mitazamo na misimamo ya nchi mbalimbali kulingana na maslahi ya nchi zao, majadiliano hayo hayakuweza kufikia muafaka na hivyo mwenyekiti wa Mkutano ndugu Luisaliaghirisha majadiliano mpaka pale atakapotangaza tarehe mpya ya kuendeleza majadiliano hayo na hatimaye kupata mkataba husika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni