Nyumbani

DKT. SEMESI AKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUDHIBITI MATUMIZI YA ZEBAKI

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware Semesi, amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Zebaki kwa Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu (EHPMP) katika maeneo mbalimbali ya uchimbaji mdogo.

Katika ziara hiyo, alitembelea mwalo wa mfano wa matumizi salama ya dhahabu unaojengwa llindi, kata ya Mwime wilayani Kahama; kituo cha teknolojia mbadala ya zebaki kijijini Bumva, kata ya Segese, Halmashauri ya Msalala; pamoja na kituo cha elimu ya kudhibiti matumizi ya zebaki kinachojengwa katika Halmashauri ya Mji wa Geita.


Aidha, Dkt. Semesi alikutana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Ndugu Mohamed J. Gombati, na kujadili changamoto za mazingira pamoja na umuhimu wa kuanzishwa kwa Ofisi mpya ya kikanda ya NEMC mkoani Geita inayohudumia mikoa ya Geita, Shinyanga na Kagera.

Dkt. Semesi pia alisisitiza ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinaendelezwa sambamba na ulinzi endelevu wa mazingira.










Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

TIMU YA UKAGUZI WA MAZINGIRA KUTOKA NEMC MAKAO MAKUU NA KANDA YA ZIWA VICTORIA MASHARIKI WAADHIMISHA MEIMOSI 2026 KWA KUPANDA MITI MAKUMBUSHO YA MWL. JULIUS K. NYERERE, BUTIAMA

Timu ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wanaofanya ukaguzi wa mazingira katika mikoa ya Kanda ya Zi...