Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Ilala limeshirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na wadau mbalimbali wa Mazingira kusafisha fukwe ya Dengu iliyopo Kata ya Kivukoni, Wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam.
Zoezi hilo lililofanyika leo Januari 31, 2026 lililenga kuimarisha usafi wa mazingira na kulinda fukwe dhidi ya uchafuzi pamoja na kuboresha mandhari ya jiji, hususan Wilaya ya Ilala ambayo ni lango kuu la kupokea wageni wanaoingia nchini kupitia Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Stesheni ya Treni.
Mgeni rasmi katika zoezi hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo, ambaye amesisitiza umuhimu wa kuendeleza usafi wa mazingira kwa ushirikiano wa karibu kati ya Serikali, taasisi na wadau mbalimbali ili kuhakikisha Wilaya ya Ilala inaendelea kuwa safi, salama na yenye kuvutia.
Amesema ushiriki wa wadau katika shughuli za usafi wa mazingira ni nguzo muhimu ya kulinda afya za wananchi, kuhifadhi mazingira ya fukwe na kuchangia maendeleo endelevu ya jiji na taifa kwa ujumla.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni