Nyumbani

NEMC YAWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WAKE KATIKA MAWASILIANO NA VYOMBO VYA HABARI

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) leo Februari 2, 2026 limewawezesha watumishi wake kwa kuwapatia mafunzo ya namna bora ya kuwasiliana na vyombo vya habari, yaliyofanyika katika ofisi za NEMC jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yalitolewa na mwezeshaji Dkt. David Mrisho (PhD) ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Umma na Masoko katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), yakilenga kuwaimarisha watumishi katika utoaji wa taarifa sahihi, zenye ujumbe mmoja na unaoeleweka kwa umma kupitia vyombo vya habari.

Katika mafunzo hayo, mwezeshaji alieleza mbinu ya “3 Key Message Rule”, inayosaidia katika uwasilishaji wa taarifa kwa kujikita kwenye maswali muhimu ya nini kilitokea, nini kinafanyika kwa sasa, na nini kitaendelea kufanyika.

Aidha, washiriki walifundishwa matumizi ya mbinu ya “bridging technique” wakati wa kujibu maswali ya waandishi wa habari, ili kuhakikisha majibu yanabaki kuakisi ujumbe mkuu wa taasisi bila kupotosha mwelekeo wa mawasiliano.

Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za NEMC za kuimarisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi wa mawasiliano ya taasisi, hususan katika masuala ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NEMC YASHIRIKI KIKAMILIFU KONGAMANO LA ANWANI ZA MAKAZI NA MAONESHO YA TEKNOLOJIA ZA POSTA 2026

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki kikamilifu Kongamano la Mwaka la Anwani za Makazi na Maonesho ya Hud...