Nyumbani

NEMC YAFANYA UFUATILIAJI WA MRADI WA KCCMP

Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya ufuatiliaji wa baada ya utekelezaji wa Mradi wa Uhifadhi na Usimamizi wa Bonde la Kihansi (KCCMP) kuanzia tarehe 19 hadi 30 Januari 2026 katika wilaya za Mlimba, Kilolo na Mufindi.

Mradi huo ulitekelezwa kati ya 2013 hadi 2019, ukiwa na lengo la kuimarisha uhifadhi wa bioanuai na kulinda viumbe hai adimu kama Chura wa Kihansi (Kihansi Spray Toad), sambamba na kusimamia rasilimali za maji kwa uendelevu.

Timu ya NEMC iliongozwa na Bw. Paul Kalokola, ikishirikiana na maafisa wa halmashauri na taasisi kama UDSM, SUA, TAWIRI, TANESCO na Ofisi ya Bonde la Rufiji. Walitembelea vituo vya uzalishaji na urejeshwaji wa Chura wa Kihansi na maeneo ya mradi kujionea utekelezaji.

Ripoti ya NEMC itatoa mapendekezo ya kitaalamu kuhakikisha uendelevu wa matokeo ya mradi na uhifadhi wa Bonde la Kihansi kwa muda mrefu.













Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NEMC YASHIRIKI KIKAMILIFU KONGAMANO LA ANWANI ZA MAKAZI NA MAONESHO YA TEKNOLOJIA ZA POSTA 2026

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki kikamilifu Kongamano la Mwaka la Anwani za Makazi na Maonesho ya Hud...