Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki Kikao cha kwanza cha kujenga Mashirikiano baina ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika Februari 17, 2026, Zanzibar.
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Festo Dugange (katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Baadhi ya watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania Bara mara baada ya Kikao cha mashirikiano kati ya pande hizo mbili. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Sware Semesi na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA) Bw. Sheha Mjaja Juma
Aidha, Kikao hicho ambacho ni mwendelezo wa Kikao kilichoanza Februari 16, 2026 kwa ngazi ya wataalamu na Februari 17 kwa ngazi ya Viongozi, kutoka Tanzania Bara kimehudhuriwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Festo Dugange (Mb), Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa pamoja na baadhi ya watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni