Nyumbani

NEMC YASHIRIKI MKUTANO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA UHIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA BAINA YA TANZANIA NA ZANZIBAR

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limeshiriki mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wenye lengo la kuleta ushirikiano kuhusu masuala ya uhifadhi na usimamizi wa Mazingira baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.


Mkutano huo umeanza Februari 16 , 2026 kwa ngazi ya wataalamu na 17 Februari, 2026 kwa ngazi ya viongozi Kisiwani Zanzibar.

Itakumbukwa kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeweka utaratibu wa wizara, Idara na Taasisi zisizo za Muungano za SJMT na SMZ zinazoshabihiana kimajukumu kufanya vikao vya kuimarisha ushirikiano ili kubadilishana uzoefu, kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji na kujadili na kushughulikia changamoto mbalimbali za kiutendaji zilizopo baina ya pande hizo mbili







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

TIMU YA UKAGUZI WA MAZINGIRA KUTOKA NEMC MAKAO MAKUU NA KANDA YA ZIWA VICTORIA MASHARIKI WAADHIMISHA MEIMOSI 2026 KWA KUPANDA MITI MAKUMBUSHO YA MWL. JULIUS K. NYERERE, BUTIAMA

Timu ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wanaofanya ukaguzi wa mazingira katika mikoa ya Kanda ya Zi...