Nyumbani

NEMC NA WATER AIDS WAADHIMISHA SIKU YA MAJI

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la WaterAid, katika kuadhimisha mwezi wa maji mwezi Machi na Siku ya urejelezaji Duniani (Global Recycling Day, tarehe 18 Machi), kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Taka Sifuri (International Day of Zero Waste), limefanya tathmini ya hali ya udhibiti wa taka ngumu kwa lengo la kulinda chanzo cha maji cha Ziwa Bassotu kilichopo Kijiji cha Bassotu, Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara.

Tathmini hiyo imelenga kubaini changamoto zilizopo na kuweka mikakati bora ya udhibiti wa taka ndani ya kijiji hicho na maeneo jirani, ili kunusuru ziwa hilo ambalo kwa sasa linakabiliwa na hatari ya kugeuzwa dampo lisilo rasmi. Hali hii inachangiwa na utupaji holela wa taka ngumu, ikiwemo chupa za viuatilifu vinavyotokana na shughuli za kilimo, jambo linalohatarisha ubora wa maji, uhai wa viumbe hai ziwani na afya ya binaadamu na mazingira kwa ujumla.

Malengo hayo yanaweza kufikiwa endapo tutaimarisha utekelezaji wa dhana ya uchumi mzunguko (circular economy) kuelekea taka sifuri kupitia urejelezaji. Hatua hii itasaidia kulinda chanzo hicho cha maji na kuboresha hali ya mazingira ya Kijiji cha Bassotu kwa ujumla.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la WaterAid-Tanza...