Nyumbani

TIMU YA UKAGUZI WA MAZINGIRA KUTOKA NEMC MAKAO MAKUU NA KANDA YA ZIWA VICTORIA MASHARIKI WAADHIMISHA MEIMOSI 2026 KWA KUPANDA MITI MAKUMBUSHO YA MWL. JULIUS K. NYERERE, BUTIAMA

Timu ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wanaofanya ukaguzi wa mazingira katika mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria, wakiongozwa na Meneja wa Utekelezaji wa Sheria, Mha. Luhuvilo B. Mwamila, waliadhimisha Sikukuu ya Wafanyakazi- Meimosi 2026 kwa kupanda miti katika Makumbusho ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Butiama.

Hatua hiyo ni ishara ya kuenzi dira ya Baba wa Taifa katika kuhifadhi mazingira na kusimamia utekelezaji wa sheria za utunzaji wa rasilimali za Taifa.










Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

𝗡𝗘𝗠𝗖 𝗬𝗔𝗞𝗨𝗧𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗔 𝗪𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗔𝗝𝗜 𝗪𝗔 𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 𝗚𝗥𝗘𝗘𝗡 𝗦𝗨𝗠𝗠𝗜𝗧 𝟮𝟬𝟮𝟲

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na ujumbe wa waandaaji wa Tanzania Green Summit (TGS), inayotarajiwa ...