Nyumbani

ELIMU YA ZIMAMOTO NA UOKOAJI YATOLEWA KWA WATUMISHI WA NEMC

Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limepokea elimu ya kinga na tahadhari ya Zimamoto na Uokoaji iliyotolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kupitia Afande Amani Hassan, Septemba 25, 2026 katika Ofisi za NEMC Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Elimu hiyo imelenga kuwawezesha watumishi wa NEMC na wananchi kutambua maeneo salama na kuchukua hatua stahiki za kujikinga dhidi ya majanga ya asili na yale yanayosababishwa na shughuli za binadamu.

Afande Amani amesisitiza umuhimu wa kuzingatia Sheria ya Zimamoto na Uokoaji ya mwaka 2007, pamoja na kuwa na vifaa muhimu vya kukabiliana na majanga ya moto, ikiwemo kizima moto na vifaa vya huduma ya kwanza

Aidha, amefundisha kwa vitendo namna ya kutumia vifaa vya kuzimia moto na kuchukua hatua sahihi kabla na baada ya kutokea kwa ajali za moto, pamoja na umuhimu wa kufahamu namba za dharura za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambayo ni 114.

 Pia, Afande Amani ametoa tahadhari kuhusu mvua za El NiƱo zinazotarajiwa kunyesha, akiwataka watumishi na wananchi kuchukua tahadhari mapema, kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa na kuzingatia maelekezo ya mamlaka husika kwa ajili ya usalama wao na mali zao.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NEMC, TNBC NA TPSF ZAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUBORESHA HUDUMA ZA EIA KWA WAWEKEZAJI

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na Kiongozi wa Tanzania National Business Council (TNBC) pamoja na Ra...