Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Mohamed Gombati tarehe 09 Novemba,2026, amekutana na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ambapo amelipongeza Baraza kwa kufungua ofisi Mkoani humo, akieleza kuwa hatua hiyo ni ya kimkakati katika kuimarisha usimamizi wa mazingira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Mkoa wa Geita.
Amekutana na uongozo huo wakati wa ukaguzi wa Jengo lililojengwa Mkoani Geita kwa aajili ya kutolea elimu ya matumizi sahihi ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo (Mazingira House)
Amesema uwepo wa ofisi hiyo utarahisisha mawasiliano na ushirikiano kati ya NEMC, Serikali na wadau mbalimbali, hususan katika kushughulikia masuala yanayohitaji utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusu utunzaji wa mazingira, ikiwemo kupunguza matumizi ya zebaki na kuhakikisha kemikali zinatunzwa na kutumika kwa kuzingatia taratibu za usalama.
Akizungumzia changamoto za uwekezaji Mkoani humo, Mohamed Gombati amebainisha kuwa baadhi ya wawekezaji, wanakabiliwa na changamoto ya kutokuzingatia kikamilifu matakwa ya Sheria na Kanuni za Mazingira (Environmental Compliance).
Ameitaka NEMC kuendelea kuimarisha usimamizi, kutoa elimu na kushirikiana na Serikali pamoja na wawekezaji ili kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinafanyika kwa kuzingatia Sheria, kulinda mazingira na kuchochea maendeleo endelevu ya Mkoa wa Geita.

.jpeg)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni