Nyumbani

MATUKIO KATIKA PICHA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe Ndug. Christopher Aloyce Sanga  wakwanza kulia akipatiwa Elimu ya Utunzaji Mazingira baada ya kutembelea Banda la NEMC katika Maonesho ya Nanenane 2025 yanayofanyika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya. Karibu banda la NEMC upate elimu ya Mazingira kwa kilimo endelevu na rafiki kwa Mazingira.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe Ndug. Christopher Aloyce Sanga alipotembelea banda la NEMC katika maonesho ya wakulima, nanenane 2025 jijini Mbeya 

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Songwe, Kidato cha Tano na cha Sita wametembelea Banda la NEMC katika maonesho ya Wakulima (Nanenane 2025) na kupatiwa elimu ya Utunzaji wa Mazingira ikiwa ni pamoja na elimu ya Utunzaji wa Mazingira inayoenda sambamba na Kilimo endelevu na rafiki kwa Mazingira, Kwa Jijini Mbeya maonesho ya Nanenane yanayofanyika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Songwe wakiwa katika banda la NEMC ambapo wamepatiwa elimu ya Utunzaji wa Mazingira katika maonesho ya nanenane 2025 jijini Mbeya 

NEMC IKO KAZINI- ELIMU YA MAZINGIRA YAENDELEA KUTOLEWA VIWANJA VYA NANENANE - DODOMA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizinw Mazingira (NEMC) limeendelea kuelimisha umma wa watanzania umuhimu wa kufanya kilimo, uvuvi na ufugaji salama unaozingatia misingi ya utunzaji Bora wa ardhi kwa maendeleo ya mazingira nchini.

Elimu hiyo inatolewa katika maonesho ya wakulima nanenane jijini Dodoma katika viwanja vya nzuguni yenye kaulimbiu isemayo " Chagua viongozi Bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi"


Timu ya NEMC ikiendelea na utoaji wa elimu ya Mazingira katika maonesho ya Wakulima, nanenane 2025 katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma 

NEMC inaendelea kuwakaribisha wadau wote wa Mazingira katika Banda lao lililopo viwanja vya Nanenane, nzuguni Dodoma, kwenye hema la tatu la Taasisi za Serikali ili kupata elimu ya mazingira kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi.



Wageni waliotembelea banda la NEMC katika maonesho nanenane 2025 wakisikiliza kwa makini elimu ya Mazingira inayotolewa na maafisa wa NEMC 


PROFESA MSOFE AZURU BANDA LA NEMC MAONESHO YA NANENANE- DODOMA

Naibu katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Peter Msofe ametembelea Banda la NEMC lililoko viwanja vya  Nanenane Nzuguni , Jijini Dodoma.

Akiwa bandani hapo, alifurahishwa na elimu ya Mazingira inayotolewa hususani ya namna bora ya kufanya kilimo, uvuvi na ufugaji unaozingatia utunzaji wa mazingira kwa mstakabali wa maendeleo endelevu nchini.

Amefurahishwa na huduma hiyo na kuitaka NEMC kuendeleza juhudi za utoaji elimu ya usimamizi na uhifadhi wa mazingira kwa mujibu wa Sheria

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira) Profesa Peter Msofe akizungumza na watumishi wa NEMC alipotembelea banda la NEMC leo 2 Agosti, 2025 katika maonesho ya wakulima (Nanenane 2025) yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma 

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Profesa Peter Msofe akisaini kitabu cha wageni  alipotembelea banda la NEMC katika maonesho ya wakulima (Nanenane 2025) yanayofanyika katika  Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma leo 2 Agosti, 2025



NEMC YAJIPAMBANUA ELIMU YA MAZINGIRA NANENANE DODOMA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeendelea kutumia Maonesho ya Kilimo ya Nanenane viwanja vya Nzuguni Dodoma, kama jukwaa muhimu la kutoa elimu ya mazingira kwa vitendo, likiwaelimisha wananchi kuhusu mbinu salama na endelevu katika sekta za kilimo, uvuvi na ufugaji.

Elimu ya mazingira inayotolewa inasisitiza matumizi ya mbinu kama kilimo hifadhi, uvuvi usioharibu makazi ya viumbe wa majini, pamoja na ufugaji usiochafua vyanzo vya maji na ardhi.

Timu ya maafisa wa NEMC wakimsikiliza mgeni aliyetembelea banda la NEMC katika maonesho ya Wakulima, nanenane 2025 katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma. Wa nne kushoto ni Kaimu Meneja Kanda ya Kati Bw. Novatus Mushi

“Tunafundisha wakulima kutumia mbinu za kuongeza tija bila kuharibu ardhi au kuchangia mmomonyoko wa udongo. Wafugaji pia wanapata maarifa juu ya ufugaji wa kisasa unaozingatia kanuni za kimazingira,” alisema mmoja wa maafisa walioko kwenye banda hilo.

Pamoja na elimu hiyo, NEMC inawakumbusha wananchi kuhusu wajibu wa kutekeleza Sheria ya Mazingira, ikiwa ni pamoja na kuzingatia Tathmini ya Athari kwa Mazingira kabla ya kuanzisha miradi mikubwa ya kilimo au ufugaji.

Mgeni aliyetembelea banda la NEMC akisaini kitabu cha wageni

Katika upande wa uvuvi, wananchi wanapewa maelezo kuhusu athari za uvuvi haramu na matumizi ya zana hatarishi kwa maisha ya majini, huku wakihimizwa kutumia mbinu salama zinazowezesha uvunaji endelevu wa rasilimali za maji.

Wakazi waliofika kwenye banda hilo wameonesha mwitikio chanya, wengi wakikiri kuwa elimu wanayopata imewafumbua macho kuhusu nafasi yao katika kulinda mazingira wanayoyategemea kwa maisha yao ya kila siku.

Maonesho ya Nanenane mwaka huu yanaendelea kuvutia taasisi mbalimbali za umma na binafsi, huku kaulimbiu ikisisitiza uchaguzi wa viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi

Elimu ya Mazingira katika kilimo endelevu na rafiki kwa Mazingira inaendelea kutolewa katika maonesho ya wakulima, nanenane 2025 katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma

PROFESA MSOFE ARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA NEMC

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi akimkabidhi zawadi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Peter Msofe mara baada ya Kikao na watumishi wa Baraza

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira)  Profesa Peter  Msofe  ameonekana kuridhishwa na utendaji kazi na uwajibikaji wa watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika utekelezaji wa majukumu ya Mazingira hasa usimamizi wa utekelezaji wa Sheria ya Mazingira Nchini.

Hayo yamedhihirika wakati alipotembelea Ofisi za Baraza jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza toka kuteuliwa kwake katika nafasi hiyo ya Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mazingira.

Amesema "NEMC pamoja na changomoto zote, bado mmepiga hatua katika suala Zima la usimamizi wa utekelezaji wa Sheria ya Mazingira nchini.

Mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Peter Msofe alipotembelea Ofisi za NEMC tarehe 31 Julai, 2025 Jijini Dar es Salaam

Amesema "NEMC  mnafanya kazi, watu wanaona na mnaonekana, licha ya changamoto mnazokumbana nazo, lakini endeleeni kufanya  kazi kwa ajili ya manufaa ya Taifa la Tanzania,  huku mkilinda Afya zenu dhidi ya  Mazingira hatarishi katika Utekelezaji wa majukumu yenu" amesema Prof.Msofe.

Aidha ameainisha mambo matano ambayo watumishi wa NEMC wanatakiwa  kuyazingatia katika utekelezaji wa majukumu ambayo ni kuweka uwiano kati ya vihatarishi binafsi na vihatarishi vya Mazingira ya kazi ili kuepuka madhara ya kiafya katika Utekelezaji wa majukumu, kujifunza na kushirikishana ujuzi wa utendaji kazi, ushirikiano mkubwa katika kazi na uvumbuzi katika maswala ya Mazingira ili kuweza kufanya kazi kwa kuendana na ulimwengu wa sasa

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Peter Msofe akizungumza katika kikao na watumishi alipotembelea Ofisi za NEMC tarehe 31 Julai, 2025. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Msofe akizungumza wakati wa Kikao na watumishi wa NEMC

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi alipozungumza ameesema bado NEMC inakabiliana na changamoto katika kutekeleza majukumu yake kutokana na kukosekana kwa Sheria inayotoa Mamlaka kamili ya Utekelezaji ambapo bado mchakato wa kuifanya NEMC kuwa Mamlaka unaendelea.

Amesema Baraza linatumia Vyombo vya ulinzi na usalama katika Utekelezaji wa baadhi ya majukumu kutokana na kukosekana kwa Mamlaka kamili.

Baadhi ya watumishi wa NEMC wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Peter Msofe wakati wa Kikao hicho

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Peter Msofe na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi wakifuatilia wasilisho kuhusu kazi na majukumu mbalimbali ya NEMC lililowasilishwa na mmoja wapo wa watumishi 

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Peter Msofe (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa NEMC mara baada ya Kikao na watumishi. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha (NEMC) Bw. Dickson Mjinja

NEMC YASHIRIKI UZINDUZI WA MFUMO WA KIDIGITALI WA KUFUTILIA UCHAFUZI WA MAZINGIRA ULIOFANYIKA MJINI ACCRA NCHINI GHANA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki uzinduzi wa mfumo wa kidigitali wa kufuatilia uchafuzi wa mazingira (Online Continuous Emissions Monitoring System) ambao umelenga kurahisisha upatikanaji wa taarifa za uchafuzi.

Uzinduzi huo uliofanyika tarehe 29 Julai 2025 mjini Accra nchini Ghana umehudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza Dkt. Immaculate Sware Semesi pamoja na Bi. Jackline Nyantori, Afisa Sheria Mkuu.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi (katikati) akiwa na baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa mfumo huo


Washiriki wa uzinduzi wa mfumo wa kidigitali wa kufuatilia uchafuzi wa Mazingira wakiwa katika Ukumbi ulipofanyika uzinduzi huo

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi (wa katikati) akiwa na baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa Mfumo huo


Picha ya pamoja ya baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa Mfumo huo 


NEMC YAPIGA MARUFUKU UCHIMBAJI WA MCHANGA MTO MPIJI KUEPUSHA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC leo 30 Julai, 2025 limepiga maarufu zoezi la Uchimbaji mchanga katika bonde la mto Mpigi unaotenganisha Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani ambalo limekuwa likiharibu Mazingira na kuhatarisha makazi ya watu wa eneo hilo kutokana na mmomonyoko wa udongo.\

Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa mto huo, Meneja Uzingatiaji wa Sheria NEMC Bw. Hamadi Taimuru amesema ni marufuku wote wanaojihusisha na Uchimbaji wa mchanga katika mto huo kwa kigezo cha kusafisha mto. Amewataka kuacha mara moja uchimbaji na kuwataka wafike katika Ofisi za NEMC ili wapatiwe vibali vyenye vigezo vya kusafisha mto na si Uchimbaji wa mchanga kwa mustakabali wa utunzaji wa Mazingira.


Meneja Uzingatiaji wa Sheria (NEMC) Bw. Hamadi Taimuru akitoa maelekezo ya marufuku ya uchimbaji mchanga katika mto mpiji wakati wa ziara ya ukaguzi wa mto huo

Amesema kwa mujibu wa Sheria, ni maarufu kuchimba mchanga mita sitini ndani mtoni kwani husababisha athari kubwa kwa Mazingira na hatari kwa makazi zikiwemo kuhama kwa mto, mmomonyoko wa udongo na kusababisha mafuriko ambayo ni hatari kwa makazi ya watu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Baraza la wazee Bw. Lazaro Silla amesema kwa niaba ya wakazi wa eneo hilo hawahitaji Uchimbaji wa mchanga katika eneo hilo kwani unasababisha uharibifu wa Mazingira na kuhatarisha usalama wa makazi yao hivyo ameiomba NEMC kudhibiti swala hilo ili lisiendelee kuleta madhara.

Timu ya NEMC ikiwa katika ziara ya ukaguzi wa mto Mpiji

Aidha, Bw. Taimuru ameongeza kuwa marufuku hii si tu kwa mto mpiji bali ni mito yote na maeneo yote nchini ambayo wanajihusisha na uchimbaji mchanga na kusababisha uharibifu wa Mazingira na kuhatarisha makazi ya watu.

Sambamba na hayo amesisitiza wote wanaojihusisha na Uchimbaji mchanga holela kote nchini kutii agizo hilo ili kuepusha uharibifu wa Mazingira na hatari ya kuharibika kwa makazi ili kujiepusha na adhabu kali inayoweza kutolewa.

Meneja Uzingatiaji wa Sheria (NEMC) Bw. Hamadi Taimuru akitoa maelekezo ya marufuku kwa baadhi ya wachimbaji mchanga katika mto Mpiji 




NEMC YASHIRIKI MKUTANO WA SABA WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU MAZINGIRA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linashiriki Mkutano wa Saba (07) wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (07th Unit...