Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika kuadhimisha Siku ya Afya mazingira Duniani, Leo tarehe 26 Septemba limetembelea Shule ya Msingi Mikocheni "A" na kutoa elimu ya Afya na Mazingira kwa wanafunzi na walimu ambapo kaulimbiu kwa mwaka huu 2025 ni "Tokomeza taka za plastiki, Jenga jamii yenye afya Bora.
Elimu hiyo imejikita katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira shuleni, pamoja na kuelezea Dhana ya Punguza, Tumia tena na Rejeleza katika Udhibiti wa taka ikiwa ni pamoja na kufundisha kuhusu usafi wa mwili na mazingira ya nyumbani.
Afisa Mazingira wa NEMC Bi. Rukia Ally akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mikocheni "A" katika Maadhimisho ya Siku ya Afya Mazingira Duniani tarehe 26, Septemba.Wanafunzi walishirikiana kwa kuuliza maswali na kujifunza mbinu rahisi za kuhakikisha mazingira yao yanabaki safi na salama kwa wote.
Aidha, maafisa hao walitoa wito kwa jamii nzima kushirikiana katika kuendeleza jitihada za kulinda mazingira, kwani afya njema haiwezi kupatikana endapo mazingira yanaharibika. Waliwataka wazazi, walimu na viongozi wa jamii kuhakikisha elimu hiyo inapelekwa hadi majumbani na maeneo ya kazi, ili kila mmoja awe balozi wa mazingira bora.
Hivyo basi, maadhimisho ya Siku hii yamekuwa chachu ya kuimarisha mshikamano wa pamoja katika kuyalinda mazingira kwa mustakabali endelevu wa kizazi cha sasa na kijacho.
Maafisa wa NEMC wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mikocheni A mara baada ya kutoa elimu ya Mazingira kwa wanafunzi wa Shule hiyo ikiwa ni sehemu ya Kuadhimisha Siku ya Afya Mazingira DunianiWanafunzi wa Shule ya Msingi Mikocheni A wakifuatilia Elimu iliyotolewa na Maafisa Mazingira kutoka NEMC katika Maadhimisho ya Siku ya Afya Mazingira Duniani