Nyumbani

DKT. MKAMA AZURU BANDA LA NEMC MAONESHO YA KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI JUNI 5

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Switbert Zacharia Mkama (Mb)

ametembelea Banda la NEMC katika maonesho ya Maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma.

Aidha, Mhe. Naibu Waziri alipozungumza, ameitaka NEMC kuongeza nguvu katika udhibiti wa maswala ya uharibifu wa Mazingira ikiwa ni pamoja na uchomaji holela wa misitu. Pia kutoa elimu kwa makundi yote ya jamii kuanzia vijana mpaka wazee, ufuatiliaji wa misitu kupitia Kanda za NEMC, kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na kuhimiza usafi kwa mito inayokabiliwa na uchafuzi.









 

Elimu ya Mazingira ikitolewa katika banda la NEMC katika Kongamano la Vijana lililofanyika katika  Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Juni 2, 2026 lenye kauli mbiu "Ushiriki wa Vijana katika Kutekeleza Dira 2050: Usimamizi Endelevu wa Mazingira na Uhimilivu wa  Mabadiliko ya Tabianchi"

WAZIRI MASAUNI AZURU BANDA LA NEMC KONGAMANO LA VIJANA LILILOFANYIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (kulia) akisikiliza maelezo katika Banda la NEMC alipotembelea Banda hilo katika Kongamano la Vijana lililofanyika katika  Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Juni 2, 2026 lenye kauli mbiu "Ushiriki wa Vijana katika Kutekeleza Dira 2050: Usimamizi Endelevu wa Mazingira na Uhimilivu wa  Mabadiliko ya Tabianchi"


Elimu ya Mazingira ikitolewa katika banda la NEMC katika Kongamano la Vijana lililofanyika katika  Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Juni 2, 2026 lenye kauli mbiu "Ushiriki wa Vijana katika Kutekeleza Dira 2050: Usimamizi Endelevu wa Mazingira na Uhimilivu wa  Mabadiliko ya Tabianchi"

NEMC YASHIRIKI KONGAMANO LA VIJANA KUJADILI USIMAMIZI ENDELEVU WA MAZINGIRA NA DIRA 2050

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeungana na wadau mbalimbali wa Mazingira kushiriki Kongamano la Vijana lililofanyika Juni 2, 2026 katika Ukumbi wa Maktaba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), likiwa na kaulimbiu isemayo "Ushiriki wa Vijana katika Kutekeleza Dira 2050: Usimamizi Endelevu wa Mazingira na Uhimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi."

Akifungua kongamano hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni, amesisitiza umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ili kuhakikisha maendeleo endelevu na utekelezaji wenye mafanikio wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.


Kupitia kongamano hilo, NEMC imepata fursa ya kutoa elimu ya mazingira kwa vijana, kuhamasisha matumizi endelevu ya rasilimali na kujadili nafasi ya vijana katika kuibua suluhisho bunifu za kukabiliana na changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa maendeleo ya Taifa ya sasa na vizazi vijavyo.





Mhandisi Adrian Kayombo akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa alipozuru Banda la NEMC Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani yanayofanyika katika viwanja vya JKCC Jijini Dodoma.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MHE. REUBEN KWAGILWA AZURU BANDA LA NEMC MAONESHO KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Reuben Kwagilwa (wa katikati kulia) azuru Banda la NEMC Maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani, katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Center (JKCC) Jijini Dodoma ambapo leo tarehe 1 Juni ndio ufunguzi wa maonesho hayo. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda.

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa (katikati kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Kati, Bw. Novatus Mushi alipozuru Banda la NEMC katika Wiki ya Maonesho kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, Juni 5 2026 yaliyofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma.