Nyumbani

"𝗡𝗘𝗠𝗖 𝗠𝗡𝗔𝗙𝗔𝗡𝗬𝗔 𝗞𝗔𝗭𝗜 𝗡𝗭𝗨𝗥𝗜" -𝗡𝗪-𝗧𝗔𝗠𝗜𝗦𝗘𝗠𝗜, 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗘𝗜𝗙

Ni kauli yake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), anayeshugulikia Afya, Dkt. Rajabu Seif, alipotembelea banda la NEMC  viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre, Jijini Dodoma kwenye maonesho ya kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika 05/06 Kila Mwaka ambayo kwa mwaka huu yanakaulimbiu isemayo Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania.


Akiwa katika banda hilo, Dkt. Seif alipongeza juhudi za NEMC katika kuelimisha wananchi kuhusu masuala ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini.

Alisema kazi inayofanywa na NEMC ina mchango mkubwa katika kuongeza uelewa wa jamii kuhusu wajibu wao wa kulinda mazingira na kuhakikisha rasilimali za asili zinatunzwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.


Katika banda hilo, wananchi wanapata elimu kuhusu umuhimu wa kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii, umuhimu wa upandaji miti, utenganishaji wa taka kuanzia kwenye chanzo, pamoja na dhana ya taka sifuri inayolenga kupunguza uzalishaji wa taka na kuongeza matumizi ya mbinu za urejelezaji. 

Dkt. Seif alisisitiza kuwa ushirikiano kati ya NEMC, taasisi mbalimbali na wananchi ni muhimu katika kufanikisha agenda ya uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira nchini inafanikiwa kwa maendeleo endelevu.

ELIMU YA MAZINGIRA IKITOLEWA KATIKA MAONESHO YA KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI JUNI 5 2026

 Elimu ya Mazingira ikiendelea kutolewa katika Banda la NEMC katika maonesho kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma 

Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 1 Juni 2026 na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa.




NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMI (AFYA) MHE. DKT. RAJAB SEIF AZURU BANDA LA NEMC KATIKA MAONESHO YA KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI anayeshughulikia Afya Mhe. Dkt. Rajab Seif azuru Banda la NEMC katika maonesho ya kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo leo ni siku ya tatu tangu kufunguliwa kwake tarehe 1Juni, 2026.






WATUMISHI WA NEMC WAKITOA ELIMU YA MAZINGIRA KATIKA WIKI YA MAONESHO KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI, JUNI 2026


Elimu ya Mazingira ikitolewa katika maonesho kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma ambapo Maadhimisho hayo yatafanyika Juni 5.








DKT. MKAMA AZURU BANDA LA NEMC MAONESHO YA KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI JUNI 5

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Switbert Zacharia Mkama (Mb)

ametembelea Banda la NEMC katika maonesho ya Maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma.

Aidha, Mhe. Naibu Waziri alipozungumza, ameitaka NEMC kuongeza nguvu katika udhibiti wa maswala ya uharibifu wa Mazingira ikiwa ni pamoja na uchomaji holela wa misitu. Pia kutoa elimu kwa makundi yote ya jamii kuanzia vijana mpaka wazee, ufuatiliaji wa misitu kupitia Kanda za NEMC, kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na kuhimiza usafi kwa mito inayokabiliwa na uchafuzi.









 

Elimu ya Mazingira ikitolewa katika banda la NEMC katika Kongamano la Vijana lililofanyika katika  Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Juni 2, 2026 lenye kauli mbiu "Ushiriki wa Vijana katika Kutekeleza Dira 2050: Usimamizi Endelevu wa Mazingira na Uhimilivu wa  Mabadiliko ya Tabianchi"

WAZIRI MASAUNI AZURU BANDA LA NEMC KONGAMANO LA VIJANA LILILOFANYIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (kulia) akisikiliza maelezo katika Banda la NEMC alipotembelea Banda hilo katika Kongamano la Vijana lililofanyika katika  Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Juni 2, 2026 lenye kauli mbiu "Ushiriki wa Vijana katika Kutekeleza Dira 2050: Usimamizi Endelevu wa Mazingira na Uhimilivu wa  Mabadiliko ya Tabianchi"

NEMC YASHIRIKI KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI-DODOMA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki kikamilifu kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliy...