Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kusini limeshiriki katika Warsha ya kuelimisha umma kuhusu uwazi na uwajibikaji katika Sekta ya Uziduaji, iliyofanyika Februari 2, 2026 katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Manispaa ya Mtwara Mikindani, mkoani Mtwara.
NEMC KANDA YA KUSINI YASHIRIKI WARSHA YA UWAJIBIKAJI SEKTA YA UZIDUAJI
NEMC YAFANYA UFUATILIAJI WA MRADI WA KCCMP
Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya ufuatiliaji wa baada ya utekelezaji wa Mradi wa Uhifadhi na Usimamizi wa Bonde la Kihansi (KCCMP) kuanzia tarehe 19 hadi 30 Januari 2026 katika wilaya za Mlimba, Kilolo na Mufindi.
Mradi huo ulitekelezwa kati ya 2013 hadi 2019, ukiwa na lengo la kuimarisha uhifadhi wa bioanuai na kulinda viumbe hai adimu kama Chura wa Kihansi (Kihansi Spray Toad), sambamba na kusimamia rasilimali za maji kwa uendelevu.
Timu ya NEMC iliongozwa na Bw. Paul Kalokola, ikishirikiana na maafisa wa halmashauri na taasisi kama UDSM, SUA, TAWIRI, TANESCO na Ofisi ya Bonde la Rufiji. Walitembelea vituo vya uzalishaji na urejeshwaji wa Chura wa Kihansi na maeneo ya mradi kujionea utekelezaji.
Ripoti ya NEMC itatoa mapendekezo ya kitaalamu kuhakikisha uendelevu wa matokeo ya mradi na uhifadhi wa Bonde la Kihansi kwa muda mrefu.
WAALAMU WA KUDHIBITI MATUMIZI YA ZEBAKI KWA WACHIMBAJI WADOGO (NEMC) NA WATAALAMU KUTOKA BENKI YA DUNIA WAKUTANA NA DKT. MUYUNGI
Timu ya wataalamu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) inayosimamia Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Zebaki kwa Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu (EHPMP) wakiongozwa na Mratibu wa mradi huo Mhandishi Dkt. Befrina Igulu wakiwa na timu ya wataalamu kutoka Benki ya Dunia wamekutana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Richard Muyungi Februari 2,2026 kwenye Ofisi zilizopo katika jengo la NHIF jijini Dodoma.
Wataalamu hao NEMC na Benki ya Dunia wamekutana na Dkt. Muyungi kwa lengo la kutathmini uendelevu wa mradi na kuhakikisha uzingatiaji wa mikataba ya kimataifa.Aidha, majadiliano yaligusia upatikanaji wa rasilimali fedha za ziada kwa ajili ya usimamizi wa taka za kielektroniki ambazo zina uhusiano wa karibu na athari za madini joto kama zebaki.
Benki ya Dunia na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Richard Muyungi kwa pamoja wamepongeza hatua zilizofikiwa katika kutimiza malengo ya msingi ya utekelezaji wa mradi huu.
#ehpmp #environmentalhealth #worldbank #mercuryfree
NEMC, HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM NA WADAU WA MAZINGIRA WASAFISHA FUKWE YA DENGU
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Ilala limeshirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na wadau mbalimbali wa Mazingira kusafisha fukwe ya Dengu iliyopo Kata ya Kivukoni, Wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam.
Zoezi hilo lililofanyika leo Januari 31, 2026 lililenga kuimarisha usafi wa mazingira na kulinda fukwe dhidi ya uchafuzi pamoja na kuboresha mandhari ya jiji, hususan Wilaya ya Ilala ambayo ni lango kuu la kupokea wageni wanaoingia nchini kupitia Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Stesheni ya Treni.
Mgeni rasmi katika zoezi hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo, ambaye amesisitiza umuhimu wa kuendeleza usafi wa mazingira kwa ushirikiano wa karibu kati ya Serikali, taasisi na wadau mbalimbali ili kuhakikisha Wilaya ya Ilala inaendelea kuwa safi, salama na yenye kuvutia.
Amesema ushiriki wa wadau katika shughuli za usafi wa mazingira ni nguzo muhimu ya kulinda afya za wananchi, kuhifadhi mazingira ya fukwe na kuchangia maendeleo endelevu ya jiji na taifa kwa ujumla.
NEMC YAWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WAKE KATIKA MAWASILIANO NA VYOMBO VYA HABARI
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) leo Februari 2, 2026 limewawezesha watumishi wake kwa kuwapatia mafunzo ya namna bora ya kuwasiliana na vyombo vya habari, yaliyofanyika katika ofisi za NEMC jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yalitolewa na mwezeshaji Dkt. David Mrisho (PhD) ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Umma na Masoko katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), yakilenga kuwaimarisha watumishi katika utoaji wa taarifa sahihi, zenye ujumbe mmoja na unaoeleweka kwa umma kupitia vyombo vya habari.
Katika mafunzo hayo, mwezeshaji alieleza mbinu ya “3 Key Message Rule”, inayosaidia katika uwasilishaji wa taarifa kwa kujikita kwenye maswali muhimu ya nini kilitokea, nini kinafanyika kwa sasa, na nini kitaendelea kufanyika.
Aidha, washiriki walifundishwa matumizi ya mbinu ya “bridging technique” wakati wa kujibu maswali ya waandishi wa habari, ili kuhakikisha majibu yanabaki kuakisi ujumbe mkuu wa taasisi bila kupotosha mwelekeo wa mawasiliano.
Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za NEMC za kuimarisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi wa mawasiliano ya taasisi, hususan katika masuala ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa.
NEMC YATAMBUA USHIRIKIANO KATI YAKE NA JESHI LA POLISI
Yashiriki mahafali ya kumi ya programu za vyuo vya polisi
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetambua mchango wa jeshi la polisi ulionao katika Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira hasa suala la ulinzi na usalama kwa maafisa wakati wa ukaguzi, kudhibiti ukaidi na kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa katika masuala ya Mazingira nchini.Hayo yamedhihirika wakati wa mahafali ya kumi ya programu za vyuo vya polisi yaliyofanyika Januari 29, 2026 katika viwanja vya chuo cha taaluma ya polisi Jijini Dar es Salaam ambapo Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt.Immaculate Sware Semesi ameshiriki.Ushiriki wake ni muhimu katika kutambua mchango ilionao wa kuimarisha utekelezaji wa Sheria za Mazingira nchini kwani uhalifu wa kimazingira kama kelele chafuzi, uharibifu wa mazingira na biashara haramu ya taka hudhibitiwa kwa ufanisi zaidi hali inayoongeza utii wa Sheria, kurahisisha uchunguzi na uwasilishaji wa kesi mahakamani.
DKT. SEMESI AKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUDHIBITI MATUMIZI YA ZEBAKI
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware Semesi, amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Zebaki kwa Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu (EHPMP) katika maeneo mbalimbali ya uchimbaji mdogo.
Katika ziara hiyo, alitembelea mwalo wa mfano wa matumizi salama ya dhahabu unaojengwa llindi, kata ya Mwime wilayani Kahama; kituo cha teknolojia mbadala ya zebaki kijijini Bumva, kata ya Segese, Halmashauri ya Msalala; pamoja na kituo cha elimu ya kudhibiti matumizi ya zebaki kinachojengwa katika Halmashauri ya Mji wa Geita.
Aidha, Dkt. Semesi alikutana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Ndugu Mohamed J. Gombati, na kujadili changamoto za mazingira pamoja na umuhimu wa kuanzishwa kwa Ofisi mpya ya kikanda ya NEMC mkoani Geita inayohudumia mikoa ya Geita, Shinyanga na Kagera.
Dkt. Semesi pia alisisitiza ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinaendelezwa sambamba na ulinzi endelevu wa mazingira.
NEMC YASHIRIKI KIKAMILIFU KONGAMANO LA ANWANI ZA MAKAZI NA MAONESHO YA TEKNOLOJIA ZA POSTA 2026
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki kikamilifu Kongamano la Mwaka la Anwani za Makazi na Maonesho ya Hud...