Nyumbani

NEMC YASHIRIKI KIKAMILIFU KONGAMANO LA ANWANI ZA MAKAZI NA MAONESHO YA TEKNOLOJIA ZA POSTA 2026

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki kikamilifu Kongamano la Mwaka la Anwani za Makazi na Maonesho ya Huduma za Posta kwa kutoa elimu ya Mazingira kwa wadau walioshiriki katika Kongamano hilo.

Kongamano hilo limehitishwa rasmi leo Februari 8, 2026 na Mgeni Rasmi Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb) ambapo ameeleza umuhimu wa matumizi ya mfumo wa Anwani za Makazi (NAPA) na kusisitiza matumizi ya mfumo huo ili kuwezesha utambuzi wa makazi na Maeneo ambayo shughuli za kiuchumi zinazohitaji ufuatililiaji zinafanyika.

Kongamano hilo  lililobeba kauli mbiu isemayo "𝘼𝙣𝙬𝙖𝙣𝙞 𝙈𝙖𝙝𝙞𝙧𝙞 𝙣𝙖 𝙐𝙗𝙪𝙣𝙞𝙛𝙪 𝙬𝙖 𝙃𝙪𝙙𝙪𝙢𝙖 𝙯𝙖 𝙋𝙤𝙨𝙩𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙐𝙠𝙪𝙖𝙟𝙞 𝙅𝙪𝙢𝙪𝙞𝙨𝙝𝙞" lilianza Februari 5 na kuhitimishwa rasmi leo Februari 8, 2026 ambapo Kongamano hilo limefanyika kuanzia Februari katika Ukumbi wa  wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

𝗡𝗘𝗠𝗖 𝗬𝗔𝗞𝗨𝗧𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗔 𝗪𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗔𝗝𝗜 𝗪𝗔 𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 𝗚𝗥𝗘𝗘𝗡 𝗦𝗨𝗠𝗠𝗜𝗧 𝟮𝟬𝟮𝟲

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na ujumbe wa waandaaji wa Tanzania Green Summit (TGS), inayotarajiwa ...