Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Peter Msofe ameonekana kuridhishwa na utendaji kazi na uwajibikaji wa watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika utekelezaji wa majukumu ya Mazingira hasa usimamizi wa utekelezaji wa Sheria ya Mazingira Nchini.
Hayo yamedhihirika wakati alipotembelea Ofisi za Baraza jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza toka kuteuliwa kwake katika nafasi hiyo ya Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mazingira.
Amesema "NEMC pamoja na changomoto zote, bado mmepiga hatua katika suala Zima la usimamizi wa utekelezaji wa Sheria ya Mazingira nchini.
Mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Peter Msofe alipotembelea Ofisi za NEMC tarehe 31 Julai, 2025 Jijini Dar es SalaamAmesema "NEMC mnafanya kazi, watu wanaona na mnaonekana, licha ya changamoto mnazokumbana nazo, lakini endeleeni kufanya kazi kwa ajili ya manufaa ya Taifa la Tanzania, huku mkilinda Afya zenu dhidi ya Mazingira hatarishi katika Utekelezaji wa majukumu yenu" amesema Prof.Msofe.
Aidha ameainisha mambo matano ambayo watumishi wa NEMC wanatakiwa kuyazingatia katika utekelezaji wa majukumu ambayo ni kuweka uwiano kati ya vihatarishi binafsi na vihatarishi vya Mazingira ya kazi ili kuepuka madhara ya kiafya katika Utekelezaji wa majukumu, kujifunza na kushirikishana ujuzi wa utendaji kazi, ushirikiano mkubwa katika kazi na uvumbuzi katika maswala ya Mazingira ili kuweza kufanya kazi kwa kuendana na ulimwengu wa sasa
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Msofe akizungumza wakati wa Kikao na watumishi wa NEMC
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi alipozungumza ameesema bado NEMC inakabiliana na changamoto katika kutekeleza majukumu yake kutokana na kukosekana kwa Sheria inayotoa Mamlaka kamili ya Utekelezaji ambapo bado mchakato wa kuifanya NEMC kuwa Mamlaka unaendelea.
Amesema Baraza linatumia Vyombo vya ulinzi na usalama katika Utekelezaji wa baadhi ya majukumu kutokana na kukosekana kwa Mamlaka kamili.
Baadhi ya watumishi wa NEMC wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Peter Msofe wakati wa Kikao hichoNaibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Profesa Peter Msofe na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi wakifuatilia wasilisho kuhusu kazi na majukumu mbalimbali ya NEMC lililowasilishwa na mmoja wapo wa watumishi