Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (IUCN), limeandaa mkutano wa Tanzania Ocean Governance Forum, unaofanyika Oktoba 15–16, 2026, katika ukumbi wa Ramada Hotel, Dar es Salaam. Mkutano huo unawakutanisha wadau kutoka taasisi za serikali na zisizo za kiserikali kujadili Usimamizi endelevu wa bahari nchini Tanzania.
Mkutano huo unaongozwa na kaulimbiu isemayo “Towards Sustainable Governance in Tanzania: Strengthening Collaboration, Policy and Action”, inayosisitiza kuimarisha ushirikiano wa kitaasisi, kuboresha utekelezaji wa sera na kuchukua hatua madhubuti katika uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za bahari, sambamba na kukuza uchumi wa buluu.
Katika mkutano huo, mada kuu tatu zimejadiliwa, ambazo ni
hali ya utekelezaji wa sera na mipango ya uchumi wa buluu, mipango ya matumizi
ya maeneo ya bahari (Marine Spatial Planning – MSP) pamoja na uvuvi na uchumi
wa buluu. Majadiliano hayo yanalenga kuimarisha utekelezaji wa sera, kuratibu
matumizi ya maeneo ya bahari na kukuza sekta ya uvuvi kwa kuzingatia uhifadhi
wa mifumo ikolojia na matumizi endelevu ya rasilimali.
Mgeni rasmi katika mkutano huo ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Bw. Zahor Kassim. Kupitia jukwaa
hili, NEMC na IUCN zinalenga kuimarisha ushirikiano wa wadau, kubadilishana
maarifa na kuwezesha maamuzi na hatua zinazozingatia sera na uhifadhi wa
mazingira ya baharini, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

.jpeg)

.jpeg)




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni