Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware Semesi, anasisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa miradi ya kaboni ili kuhakikisha inalinda mazingira, inavutia uwekezaji na kuwanufaisha wananchi.
Akishiriki katika Mkutano wa Carbon Market Africa Summit
2026, uliofanyika Kigali Rwanda, Mkurugenzi Mkuu anasisitiza kuwa Tanzania ina
fursa kubwa ya kukuza soko la kaboni kupitia uhifadhi wa misitu, mikoko, mifumo
ikolojia ya bahari, urejeshaji wa ardhi na usimamizi bora wa taka.
NEMC ina jukumu muhimu katika usimamizi wa mazingira na ufuatiliaji wa uzingatiaji wa matakwa ya mazingira katika miradi ya maendeleo, ikiwemo miradi ya kaboni, kwa mujibu wa sheria na mamlaka yake.
NEMC inahimiza uwazi, uwajibikaji, ufuatiliaji wa matokeo ya
kimazingira na ushirikishwaji wa jamii ili kuhakikisha kuwa miradi ya kaboni
inachangia kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi bila kuathiri haki na
maslahi ya wananchi.
“Soko la kaboni linapaswa kuwa fursa ya kulinda mazingira, kuvutia uwekezaji wa kijani na kuboresha maisha ya wananchi. Ni muhimu kuhakikisha kuwa kila mradi unazingatia sheria, unalinda mifumo ikolojia na kuleta manufaa yanayopimika kwa jamii.”
Kupitia usimamizi madhubuti wa mazingira, NEMC itaendelea
kutekeleza wajibu wake katika kujenga mazingira wezeshi kwa uwekezaji endelevu
na kuchangia maendeleo ya kijani nchini Tanzania.










Hakuna maoni:
Chapisha Maoni