Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na kujadili utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2026/27 katika sekta ya Madini.
Katika wasilisho hilo, masuala ya udhibiti wa athari za kimazingira zitokanazo na shughuli za uchimbaji madini, usimamizi wa taka migodini, urejeshaji wa maeneo yaliyoathiriwa na uchimbaji pamoja na ufuatiliaji wa uzingatiaji wa Sheria na Kanuni za mazingira ni miongoni mwa maeneo muhimu yanayohitaji kupewa kipaumbele katika mipango na utekelezaji wa bajeti.
Kamati imeelekeza kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya NEMC na wadau wa sekta ya Madini katika kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinafanyika kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira na misingi ya maendeleo endelevu.
Majadiliano hayo yanalenga kuimarisha usimamizi wa mazingira ili rasilimali za madini ziendelee kuchangia maendeleo ya taifa huku mazingira yakilindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.



.jpeg)
.jpeg)


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni