Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linashiriki kikamilifu katika Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12), unaofanyika tarehe 6 hadi 9 Oktoba 2026 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania. Mkutano huo unaofanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 40 ya Mkataba wa Nairobi umebeba kaulimbiu “Towards Sustainable Blue Economy in the Western Indian Ocean Region for People and Nature: A Journey of Forty Years.”
Ushiriki wa NEMC unaakisi jukumu lake la kisheria na kitaalamu katika usimamizi na uhifadhi wa mazingira, ikiwemo udhibiti wa uchafuzi, tathmini ya athari za kimazingira, uzingatiaji wa viwango vya mazingira na ulinzi wa mifumo ikolojia ya bahari na pwani. Kupitia COP12, NEMC inawakilisha masuala ya mazingira ya Tanzania katika majadiliano ya kikanda kuhusu uchafuzi wa bahari, mabadiliko ya tabianchi, uhifadhi wa bioanuai na matumizi endelevu ya rasilimali za bahari.
Aidha, NEMC inatumia jukwaa hilo kuimarisha ushirikiano na
taasisi za kitaifa, kikanda na kimataifa kwa kubadilishana uzoefu, utaalamu na
teknolojia katika usimamizi wa mazingira. Ushirikiano huo ni muhimu katika
Kwa NEMC, COP12 ni fursa muhimu ya kujenga na kuimarisha
ushirikiano na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa, hususan katika
utekelezaji wa majukumu ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni